BEIJING - China itaendelea kuongeza mshikamano na ushirikiano na nchi za Latini Amerika, na kutoa hali nzuri zaidi ya kuridhika na furaha kwa watu wa pande zote mbili, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Lin Jian amesema Jumatano. Akizungumza kuhusu midoli ya alpaca va Peru, "warmpaca," kuwa moja ya bidhaa moto moto kwenye Maonyesho ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE) ya mwaka huu, msemaji Lin amesema kwamba fundi wa Sanaa za mikono wa Peru, Oswaldo Mamani ambaye awali alikuwa na karakana ya ghorofa moja kwenye jengo la maghorofa mengi na mauzo ya kila mwaka ya vitu zaidi ya 100, lakini sasa karakana yake inachukua ghorofa tatu huku mamia ya mafundi wa kazi za mikono wakijiunga naye.
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping ameondoka Beijing leo Novemba 13 kwa kuhudhuria Mkutano wa 31 wa Viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi APEC huko Lima, Peru na kufanya ziara ya kiserikali nchini Peru kutokana na mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Peru Dina Ercilia Boluarte Zegarra. Watu wanaoambatana na Rais Xi katika ziara yake hiyo ni Cai Qi, Mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Ofisi Kuu ya Kamati Kuu ya CPC, na Wang Yi, Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa China.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Hua Chunying ametangaza kuwa rais Xi Jinping wa China atahudhuria mkutano usio rasmi wa 31 wa wakuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi wa Asia na Pasifiki APEC mjini Lima na kufanya ziara nchini Peru kuanzia Novemba 13 hadi 17 kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Peru Dina Ercilia Boluarte Zegarra. Rais Xi pia atahudhuria mkutano wa 19 wa wakuu wa G20 huko Rio de Janeiro na kufanya ziara nchini Brazil kuanzia Novemba 17 hadi 21 kwa mwaliko wa Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva.
Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bi. Mao Ning jana amesema, kuanzia Maoneshao ya kwanza ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa(CIIE) kufanyika nchini China, nchi nyingi zilizo nyuma kiuchumi zimepata fursa ya kushiriki maoneshao hayo kwa urahisi.