BEIJING - Biashara kati ya China na Brazil imeongezeka kwa asilimia 9.9 katika kipindi cha miezi 10 ya kwanza ya Mwaka 2024 kuliko kipindi kama hicho mwaka jana, ikionyesha kuimarika kwa uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya nchi hizo mbili.
Rais Xi Jinping wa China akiwasili Rio de Janeiro kwa kuhudhuria kwenye Mkutano wa Kilele wa 19 wa Viongozi wa G20 na ziara ya kiserikali nchini Brazil kutokana na mwaliko wa Rais Luiz Inacio Lula da Silva, Novemba 17, 2024. (Xinhua/Ding Haitao) RIO DE JANEIRO - Rais wa China Xi Jinping amesema anatarajia kubadilishana mawazo kwa kina na Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva juu ya kuimarisha zaidi uhusiano kati ya China na Brazil, kuhimiza kuoana kwa mikakati ya maendeleo ya nchi hizo mbili, na masuala ya kimataifa na kikanda yanayofuatiliwa nao kwa pamoja.
RIO DE JANEIRO - Rais wa China Xi Jinping amewasili Rio De Janeiro, Brazil jana siku ya Jumapili kwa kuhudhuria kwenye Mkutano wa 19 wa Kilele wa G20 na kufanya ziara ya kiserikali nchini Brazil kutokana na mwaliko wa Rais Luiz Inacio Lula da Silva. Rais Xi Jinping wa China akiwasili Rio de Janeiro kwa kuhudhuria kwenye Mkutano wa 19 wa G20 na kufanya ziara ya kiserikali nchini Brazil kutokana na mwaliko wa Rais Luiz Inacio Lula da Silva, Novemba 17, 2024.
Rais Xi Jinping wa China akitoa hotuba muhimu isemayo "Kubeba Wajibu wa Nyakati Zetu na Kuhimiza kwa Pamoja Maendeleo ya Asia na Pasifiki" kwenye Mkutano wa 31 wa Viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya APEC uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Lima cha Peru, Novemba 16, 2024. (Xinhua/Xie Huanchi) LIMA - Rais wa China Xi Jinping ametangaza Jumamosi kuwa China itakuwa mwenyeji wa mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Asia Pasifiki (APEC) Mwaka 2026, na inapenda kushirikiana na pande zote ili kuzidisha ushirikiano wa Asia na Pasifiki.