人民网首页

Habari

Ajenda iliyopendekezwa ya mkutano wa mwaka wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China watangazwa

BEIJING - Ajenda iliyopendekezwa ya mkutano wa nne wa wajumbe wote wa Kamati ya 14 ya kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC), ambalo ni chombo cha juu cha mashauriano ya kisiasa cha China, imetangazwa rasmi jana Jumapili. Mkutano huo wa nne wa CPPCC utafunguliwa rasmi Machi 4 mjini Beijing, kwa mujibu wa uamuzi uliofanywa kwenye kikao cha Kamati ya Kudumu ya kamati ya kitaifa ya baraza hilo siku hiyo ya Jumapili.

Dong Hongtao (kulia) na mfanyakazi mwenzake wakikagua na kuifanyia matengenezo treni ya mwendo-kasi kwenye karakana ya matengenezo ya Kampuni ya Kundi la Reli la Xi’an la China,  katika Mkoa wa Shaanxi, kaskazini magharibi mwa China, Januari 14, 2026. (Xinhua/Li Yibo)

Fundi mwandamizi wa treni afuatilia zaidi kujiendeleza kwa vipaji vijana wa kazi ya ufundi

Dong Hongtao ni fundi wa treni za mwendo-kasi wa Kampuni ya Kundi la Reli la Xi'an la China, ambaye pia ni mjumbe wa Bunge la Umma la China (NPC). Tangu ajiunge na kazi ya matengenezo ya treni za mwendo-kasi (EMU) mwaka 2007, Dong amekuwa akiongoza timu yake kufanyia matengenezo seti zaidi ya 120,000 za treni hizo na kushughulikia hitilafu zaidi ya 3,000.

Kituo cha Vyombo vya Habari cha Mikutano Mikuu Miwili ya Mwaka ya China 2026 chafunguliwa

Kituo cha Habari cha Mkutano wa Nne wa Bunge la Umma la 14 la China (NPC) na Mkutano wa Nne wa Baraza la 14 la Mashauriano ya Kisiasa la China (CPPCC), ambayo inafahamika kwa jina la “Mikutano Mikuu Miwili ya Mwaka ya China” kimefunguliwa rasmi leo Ijumaa mjini Beijing, na kinatarajiwa kutoa huduma kwa waandishi wa habari wa ndani na nje ya nchi watakaofuatilia. Mikutano hiyo inatarajiwa kuanza mjini Beijing Machi 5 na Machi 4, mtawaliwa.

Iliyopita3 4 5 6 7