人民网首页

Habari

Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China laanza mkutano wa mwaka

Mkutano wa nne wa Kamati ya Kitaifa ya 14 ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC) ukifunguliwa katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Machi 4, 2026. (Xinhua/Yan Yan) BEIJING - Kamati ya Kitaifa ya 14 ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC), chombo cha juu cha mashauri ya kisiasa cha China, imefanya mkutano wake wa nne wa mwaka kuanzia jana Jumatano mjini Beijing ambapo Rais Xi Jinping na viongozi wengine wa Chama na serikali, wakiwemo Li Qiang, Zhao Leji, Cai Qi, Ding Xuexiang, Li Xi na Han Zheng, walihudhuria kwenye ufunguzi wa mkutano huo katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing.

Tume ya utendaji wa mkutano yachaguliwa, na ajenda za mkutano wa Bunge la Umma la China zapitishwa

Zhao Leji, mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge la Umma la China akiongoza kikao cha maandalizi ya mkutano wa nne wa Bunge hilo la 14 kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing Machi 4, 2026. (Xinhua/Shen Hong) BEIJING – Wajumbe wa Bunge la 14 la Umma la China (NPC) wamekusanyika Beijing jana Jumatano kwenye kikao cha maandalizi ya mkutano wa mwaka wa bunge hilo, ambapo wamechagua wajumbe wa tume ya utendaji wa mkutano wa mwaka na kupitisha ajenda za mkutano huo uliopangwa kuanza leo Alhamisi.

(Picha/Xinhua)

Mkutano wa mwaka wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China wafunguliwa Beijing

Mkutano wa mwaka wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China umefunguliwa rasmi leo Machi 4 saa tisa mchana katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing. Katika mkutano wa siku saba, wajumbe 2,078 kutoka nyanja 34 ikiwemo uchumi, utamaduni, elimu na raslimali za mazingira watasikiliza na kupitia ripoti ya kazi ya baraza hilo na ripoti kuhusu kazi ya utoaji mapendekezo, huku wakihudhuria mkutano wa mwaka wa Bunge la Umma la Taifa, kusikiliza na kujadili ripoti ya kazi ya serikali na ripoti nyingine husika, kujadili mswada wa mwongozo wa Mpango wa 15 wa Miaka Mitano wa Maendeleo ya Uchumi na Jamii.

Jin Ruirui akipanga mavazi ya kabila la Wayi yenye darizi  zilizofanywa kwa mikono kwenye studio yake katika Wilaya ya Mouding, Mkoa wa Yunnan, kusini magharibi mwa China, Februari 9, 2026. (Xinhua/Chen Xinbo)

Habari picha: Mjumbe wa Bunge la Umma la China aufanya ufundi wa udarizi wa kikale wa kabila la Wayi kuwa wa kisasa

Jin Ruirui, mkuu wa shirikisho la mafundi wa kudarizi la kabila la Wayi la ngazi ya kiwilaya katika Mkoa wa Yunnan, kusini magharibi mwa China, amekuwa akijikita katika kuhifadhi ufundi huo wenye historia ya miaka zaidi ya elfu moja, wakati huohuo amewaongoza mafundi wenyeji wa kudarizi kuelekea ustawi wa kitamaduni na ustawishaji wa vijiji. Ufundi huo wa kudarizi wa kabila la Wayi wenye historia ya miaka ya zaidi 1,300, unajulikana kwa udarizi wake wa michoro na picha za kupendeza na mbinu mbalimbali za kudarizi, na umekuwa kibebaji muhimu cha utamaduni wa kabila la Wayi.

Iliyopita3 4 5 6 7 Inayofuata