Lugha Nyingine
Ajenda iliyopendekezwa ya mkutano wa mwaka wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China watangazwa
BEIJING - Ajenda iliyopendekezwa ya mkutano wa nne wa wajumbe wote wa Kamati ya 14 ya kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC), ambalo ni chombo cha juu cha mashauriano ya kisiasa cha China, imetangazwa rasmi jana Jumapili.
Mkutano huo wa nne wa CPPCC utafunguliwa rasmi Machi 4 mjini Beijing, kwa mujibu wa uamuzi uliofanywa kwenye kikao cha Kamati ya Kudumu ya kamati ya kitaifa ya baraza hilo siku hiyo ya Jumapili.
Ajenda ya mkutano huo ni pamoja na kusikiliza na kujadili ripoti ya kazi ya Kamati ya Kudumu ya Kamati ya kitaifa ya baraza hilo, na ripoti kuhusu hali ya kushughulikia mapendekezo waliyoyatoa wajumbe wa baraza hilo tokea mkutano wa tatu wa wajumbe wote wa baraza hilo uliopita.
Wajumbe wa baraza hilo watakaa kwenye mkutano wa nne wa Bunge la Umma la 14 la China ili kusikiliza na kujadili nyaraka ikiwa ni pamoja na ripoti ya kazi ya serikali.
Kutokana na ajenda ya mkutano, wajumbe wa baraza hilo watajadili pia mswada wa mwongozo wa Mpango wa 15 wa Maendeleo ya Uchumi na Jamii ya Miaka Mitano (2026-2030).
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



