Lugha Nyingine
Mkutano wa mwaka wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China kufanyika Machi 4 hadi 11

Liu Jieyi, msemaji wa mkutano wa nne wa Kamati ya Kitaifa ya 14 ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC), akihudhuria mkutano na waandishi wa habari kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Machi 3, 2026. (Xinhua/Wang Xi)
BEIJING - Kamati ya Kitaifa ya 14 ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC), ambacho ni chombo cha juu cha ushauri wa kisiasa cha China, itafanya mkutano wake wa nne wa mwaka Tarehe 4 hadi Tarehe 11 mwezi huu mjini Beijing, msemaji wa mkutano huo Liu Jieyi amesema.
Mkutano huo utafunguliwa leo Tarehe 4 saa 9 alasiri (kwa saa za Beijing) na utafungwa asubuhi ya Tarehe 11 mwezi huu, msemaji Liu amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jana Jumanne.
Msemaji huyo amesema wakati wa mkutano huo, wajumbe wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China watasikiliza, kujadili na kupitisha ripoti ya kazi ya Kamati ya Kudumu ya baraza hilo, na ripoti juu ya hali ya kushughulikia mapendekezo ya wajumbe wa baraza hilo.
"Wajumbe wa baraza hilo watakuwa wasikilizaji kwenye mkutano wa nne wa Bunge la 14 la Umma la China utakaofunguliwa kesho Tarehe 5, bunge ambalo ni chombo cha juu cha nchi cha utungaji wa sheria, ambapo wajumbe wa baraza hilo watasikiliza, kujadili na kupitisha ripoti ya kazi ya serikali, na kujadili mswada wa Mpango wa 15 wa Maendeleo ya Uchumi na Jamii ya Miaka-Mitano" Liu amesema.
Amesema, pia wajumbe wa baraza hilo watathibitisha na kupitisha azimio la kisiasa la mkutano wa mwaka, azimio juu ya ripoti ya kazi ya Kamati ya Kudumu ya baraza hilo, azimio juu ya ripoti kuhusu hali ya kushughulikia mapendekezo tangu mkutano wa tatu wa mwaka uliopita, pamoja na ripoti juu ya mapendekezo mapya yaliyowasilishwa kwenye mkutano wa mwaka huu.
Amesema mkutano wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China wa mwaka 2026 utahusisha mkutano wa kufunguliwa na mkutano wa kufugwa, mikutano ya makundi na ya mashauriano ya mada maalumu. Na mabalozi wa nchi mbalimbali nchini China wataalikwa kusikiliza na kufuatilia mikutano ya kufunguliwa na kufungwa.
Kwa kutazama siku za baadaye, kazi za kufanya mashauriano, majadiliano na uangalizi wa kidemokrasia za wajumbe wa baraza hilo zitawekwa mkazo katika kusaidia nchi kuhakikisha kupata mwanzo mzuri wa utekelezaji wa Mpango wa 15 wa Miaka Mitano (2026-2030), msemaji huyo amesema.
Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China linafanya kazi muhimu katika ushirikiano wa vyama vingi na mashauriano ya kisiasa chini ya uongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC). Wajumbe wake wanatoka katika vyama mbalimbali vya kisiasa, mashirika ya umma, watu wasio na vyama na watu wa sekta mbalimbali za jamii. Kazi kuu za baraza hilo ni kufanya mashauriano ya kisiasa, usimamizi wa kidemokrasia, na kushiriki na kufanya mashauriano katika mambo ya nchi.

"Tamasha la Maolong" la kabila la Wayilao lasherehekewa kwa ngoma ya dragoni mkoani Guizhou, China

Mji mkongwe wa Wuzhen, China wazindua shughuli mbalimbali wakati wa Mwaka Mpya wa Jadi wa China

Hong Kong Yasherehekea Mwaka Mpya wa Jadi wa Farasi wa China kwa Maonyesho ya Fataki

Ufunguzi ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Milan-Cortina mwaka 2026
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma