Mgahawa wa teknolojia ya akili bandia wafurahisha zaidi wateja (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 24, 2021
Mgahawa wa teknolojia ya akili bandia wafurahisha zaidi wateja
(Picha zinatoka: cfp)

Jikoni, mikono ya roboti inachukua vitoweo kutoka rafu; kwenye ukumbi, roboti zinapeleka vitoweo mezani mwa wateja…… Hii ni hali ya kawaida kwenye migahawa mingi ya teknolojia ya akili bandia. Katika miaka ya hivi karibuni, migahawa ya kujiendesha, ya teknolojia ya akili bandia, na isiyo na wahudumu inastawi sana siku hadi siku, na imekuwa wimbi la kuboresha shughuli na kuinua kiwango kwa migahawa..

Mgahawa wa ainia hii mpya inaonesha nini “teknolojia ya akili bandia”? Twende tukatazame mgahawa wa Mchemsho wa Haidilao , ulioko kwenye eneo la Chaoyang, Beijing.

Kwa kupitia madirisha, tunaweza kuona ndani ya jiko kuna mikono kadhaa ya roboti inanyoosheka taratibu mbele ya rafu za kuwekea vitoweo, hii ni mashine ya kujiendesha ya kutoa vitoweo. Baada ya wateja kuagiza chakula, mfumo wa komputa utapasha habari kwa mashine ili itoe chakula, halafu mikono ya roboti itabeba vyakula na kuvipeleka. Hii imepunguza sana kazi zilizofanywa na wahudumu awali. 

Wateja wakifika sehemu ya kula chakula, wanaweza kupata huduma zaidi za teknolojia ya akili bandia: ukuta wa pande nne unaonesha picha ya anga buluu, mawingu meupe na maua ya sakura ya rangi ya pinki; chini ya meza kuna mfumo wa kutolea upepo nje kiteknolojia, mvuke wa mchemsho utavutwa kutoka chini moja kwa moja; na mashine ya teknolojia ya akili bandia ya kupika supu za aina mbalimbali zilizoagizwa na wateja inatoa huduma kwa “wateja elfu moja wanaotakaladha za aina mbalimbali”, wateja wanaweza kuagiza supu kutokana na ladha wanayoipenda.

Kulingana na mgahawa wa kawaida, huduma za mgahawa wa aina hii zinafaa zaidi kukidhi mahitaji tofauti ya wateja, zinaweza kuwafanya wateja kufurahia zaidi kula chakula kwenye mgahawa wa teknolojia ya akili bandia.

(Wahariri wa tovuti:Li Yidan,Zhao Jian)

Picha