Chakula bora na kitamu cha Tibet chaonyesha ladha nzito ya mshikamano wa watu na utamaduni wa Tibet (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 05, 2021
Chakula bora na kitamu cha Tibet chaonyesha ladha nzito ya mshikamano wa watu na utamaduni wa Tibet
Katika mgahawa wa chai wa Sangqu, mtaa wa Bakuo, kiini cha mji wa Lhasa, mhudumu anachukua chai kwa wateja
(Picha zinatoka: Tovuti ya Shirika la Habari la Xinhua)

Chai, ni mahitaji ya lazima kwenye maisha ya Watibet, kila siku ya kila familia ya Watibet inaanza kwa kunywa chai cha maziwa ya siagi.

Katika mtaa wa Bakuo, kiini cha mji wa Lhasa, kila siku wateja wanajaa mgahawa wa chai wa Sangqu. Supu ya ng’ombe inachemka kwenye chungu, watu wanaokaa kwenye meza wanapiga soga huku wakicheka kwa furaha, hata unaweza kuona mama mzee anayeona raha starehe baada kunywa chai…… hayo yote yameonyesha hali ya kawaida ya kuvutia katika maisha ya watu wanaoishi kwenye uwanda wa juu.

Bwana Zhang Quanlu anakula bakuli moja ya tambi ya Kitibet na kunywa chupa moja ya chai, anaona raha sana. Alisema “Kufungua kinywa cha Kitibet ni kitamu sana tena ni chakula bora kwa afya.” Bwana Zhang amefanya biashara Tibet kwa zaidi ya miaka kumi, ambapo mzaliwa huyu wa mji wa Chengdu, Sichuan amezoea maisha ya Lhasa.

“Kila siku nakuja mgahawani, naweza kujionea mila na desturi za Tibet hapa.”

Kikombe kimoja cha chai kinaonekana ni cha kawaida, kihalisi kinaonyesha historia ndefu na hisia za watu, chai moto cha maziwa ya siagi kinanukia harufu ya mshikamano wa makabila.

Ilipofika mwaka 1963, Tibet ilikuwa imepata shamba la kwanza la chai, zamani mahitaji ya chai yalitegemea uchukuzi wa makundi ya farasi kutoka mikoa ya Yunnan, Sichuan na Shan’xi kupitia njia ya kale ya farasi waliobeba chai kuyapeleka hadi Tibet. Katika utafiti wa vitu vya kale, kwenye makaburi ya Gurujiamu, wilaya ya Gar ya eneo la Ali, yalifukuliwa mabaki ya kale pamoja na chai kutoka eneo la katikati ya nchi miaka 1800 iliyopita.

Katika mamia ya miaka iliyopita, makundi ya farasi yalipita milima mirefu na bonde la chini kusini na kaskazini, nyayo za farasi na punda zimeonekana kwenye njia moja moja. Njia ya kale ya farasi waliobeba chai na njia ya kale ya biashara ya Tangfan kwenye Paa la dunia, si kama tu zilisafirisha chai, sukari nyekundu na vyombo vya mahitaji ya kila siku kutoka eneo la ndani ya nchi hadi Tibet, bali pia zilishuhudia maunganyiko ya utamaduni wa chakula wa makabila mbalimbali.

Maendeleo ya hali motomoto ya migahawa, yanawafanya wakulima na wafugaji wengi zaidi wa Tibet washiriki pia kwenye shughuli za migahawa. Hivi leo, watu wengi wa tarafa ya kabila la Wanaxi ya Yanjing wanapamba vizuri nyumba zao ili kuendesha hoteli vijijini, na kupata ongezeko la mapato.

Watu wanategemea chakula. Utamaduni wa chakula wa Tibet unaendelezwa na kuwa aina mbalimbali kutokana na mawasiliano na maingiliano kati ya makabila mbalimbali katika mamia ya miaka iliyopita, chakula bora na kitamu cha Tibet kinaonyesha mshikamano wa watu wa makabila mbalimbali.

(Wahariri wa tovuti:Li Yidan,Zhao Jian)

Picha