Polisi wanawake wa kupanda farasi, hali inayowavutia watu kwenye mbuga wa Zhaosu (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 19, 2021
Polisi wanawake wa kupanda farasi, hali inayowavutia watu kwenye mbuga wa Zhaosu
Katika jeshi la polisi wa askari wa usafiri la wilaya ya Zhaosu, kikosi cha polisi wanawake wa kupanda farasi kinafanya mazoezi ya kutoa ishara ya kuelekeza magari barabarani.
(Picha inatoka tovuti ya Shirika la Habari la China Xinhua.)

Ikiwa kadi nyingine ya Mbuga wa Zhaosu, kikosi cha polisi wanawake wa kupanda farasi cha jeshi la askari wa usafiri la ofisi ya polisi ya wilaya ya Zhaosu ya mkoa wa Xinjiang kimevutia watu sana. Polisi wanawake 15 wanaotoka makabila matano tofauti wanabeba majukumu ya kutatua hali ya msungamano barabarani, kushughulikia vitendo vya kinyume cha sheria ya usafiri, na kufanya doria kwenye maeneo ya mifugo na vivutio, ambapo ni taabu kwa magari kuingia ndani. Polisi hao wanawake wenye hali ya ukakamavu wanafanya jitihada kubwa zenye taabu zisizojulikana. Siku zote polisi wa kikosi hiki wanavaa helmeti, kupanda farasi na kufanya mazoezi wakiwa wanakabiliwa na jua kali au mvua na upepo mkubwa, ili kupata ustadi wa kupanda farasi kwa kasi na kuonyesha hali nzuri kabisa.

Tangu kilipoanzishwa mwaka 2013, kikosi cha polisi wanawake wa kupanda farasi kimetoa huduma zao mara kwa mara wakati wa majira ya utalii na kwenye shughuli kubwa. Hivi sasa polisi wanawake wanaovaa sare wanapanda farasi wakitembea kwenye mbuga na kutoa huduma kwa watalii na wafugaji.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha