Mji wa Quanzhou wafaulu kuongezwa kwenye orodha ya urithi wa dunia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 26, 2021
Mji wa Quanzhou wafaulu kuongezwa kwenye orodha ya urithi wa dunia
(Picha inatoka tovuti ya Chinadaily.)

Tarehe 25, mradi wa China wa "Mji wa Quanzhou: kituo cha biashara kwenye bahari ya dunia cha China katika Enzi za Song na Yuan" ulithibitishwa bila matatizo kwenye mkutano wa 44 wa urithi wa dunia, na umeongezwa kwenye "orodha ya urithi wa dunia", na umekuwa urithi wa dunia wa 56 ulioko China.

Mji wa Quanzhou ulioko sehemu ya pwani ya kusini ya mkoa wa Fujian wa China, uliitwa "Citong" katika zama za kale. Mji huo umekuwa na historia ya zaidi ya miaka 1300. Katika Enzi za Song na Yuan, mji wa Quanzhou ulikua katika hali motomoto ya ustawi wa biashara kwenye bahari ya kimataifa, ukawa "bandari kubwa zaidi ya dunia ya mashariki", ambapo ulikusanyika kwa wafanyabiashara na watalii kutoka nchi nyingi waliowasiliana vizuri wakiwa na utamaduni wa aina mbalimbali. Wafanyabiashara na watalii hao pamoja na wamisionari walifika Quanzhou kwa kupitia njia ya hariri ya baharini, na mpaka sasa watu wa vizazi vyao bado wanaishi huko. Utamadani wa aina mbalimbali kutoka Uajemi wa kale, Uarabu, India na Asia ya Kusini Mashariki ulifungamanishwa na utamaduni wa China katika Mji Quanzhou, na ukachangia sifa wazi ya anuwai ya jamii, kufungua mlango na shirikishi ya mji huo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha