Wilaya ya Xiuning ya Anhui: fundi wa saa wa Anhui mlinzi wa wakati (7)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 30, 2021
Wilaya ya Xiuning ya Anhui: fundi wa saa wa Anhui   mlinzi wa wakati
Picha ilipigwa na Shi Yalei

Katika mji wa Xikou wa wilaya ya Xiuning wa mji wa Huangshan, mkoani Anhui, kuna fundi mmoja wa saa anayejulikana sana huko , jina lake Cheng Gengxin.

Mwaka 1961, Cheng Gengxin alipokuwa na miaka 15 alianza kujifunza utengenezaji wa saa, chini ya msaada wa baba yake, alifanya mazoezi mengi, akapata uwezo mzuri wa kimsingi, baadaye akawa fundi maarufu wa saa katika mji huo mdogo, na amefanya kazi ya utengenezaji wa saa kwa miaka 45.

Kutokana na matumizi ya simu ya mkononi na bidhaa nyingine za elektroniki, shughuli ya utengenezaji wa saa imedidimia siku hadi siku, vijana wanaopenda kujifunza ufundi huo kwa makini wamekuwa wachache zaidi, lakini Cheng Gengxin anapenda zaidi kufanya kazi hiyo, anatumai ufundi wa utengenezaji wa saa unaweza kama saa inavyoenda bila kusita, na ufundi wake unaweza kuenea na kurithiwa daima.

(Wahariri wa tovuti:Li Yidan,Zhao Jian)

Picha