Ushirikiano katika Teknolojia ya Juncao waonesha ahadi ya kutafuta maendeleo kwa pamoja

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 06, 2021
Ushirikiano katika Teknolojia ya Juncao waonesha ahadi ya kutafuta maendeleo kwa pamoja
Profesa Lin Zhanxi anaangalia uyoga uliopandwa kwa kutumia teknolojia ya Juncao.
(Picha zinatoka tovuti ya Shirika la Habari la China Xinhua.)

Septemba 2, Rais Xi Jinping alituma salamu za pongezi kwa Maadhimisho ya Miaka 20 ya utoaji wa msaada wa Teknolojia ya Juncao pamoja na Baraza la ushirikiano wa kimataifa wa kusaidia maendeleo endelevu, akisifu teknolojia ya Juncao kwa mchango wake mkubwa katika ushirikiano wa kimataifa.

Rais Xi alisema, Teknolojia ya Juncao ni njia ya kupanda uyoga na mazao ya chakula cha mifugo kwenye nyasi zilizokatwa, hii ni njia pekee iliyovumbuliwa na China.

Profesa Lin Zhanxi mwenye umri wa miaka 78 amesifiwa kuwa “Baba wa Juncao duniani”, alivumbua teknolojia hiyo ambayo si kama tu imewasaidia mamia na maelfu ya wakulima kuondokana na umaskini baada ya kupanda uyoga, bali pia imetoa mchango mkubwa katika kulinda mazingira ya asili.

Mwaka 1983, ili kuwasaidia wakulima wa China wajitoe kutoka kwenye lindi la umaskini, Bwana Lin aliacha wadhifa wake katika chuo kikuu na kuanza kutafiti teknolojia ya kupanda uyoga.

Baada ya juhudi za miaka kadhaa, alifanikisha utafiti wake. Hivi sasa Teknolojia ya Juncao imeenezwa katika nchi 106 duniani, na vituo vya kielelezo vya kupanda uyoga vimeanzishwa katika nchi 13 zikiwemo Papua New Guinea, Fiji, Rwanda na nyinginezo, na kuleta nafasi za ajira laki kadhaa za shughuli zisizochafua mazingira kwa ajili ya vijana na akinamama. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha