Mji wa Hengzhou, mkoani Guangxi: Harufu ya maua ya jasmine yaonesha hatua ya ustawishaji wa vijijini (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 06, 2021
Mji wa Hengzhou, mkoani Guangxi: Harufu ya maua ya jasmine yaonesha hatua ya ustawishaji wa vijijini

Mji wa Hengzhou, mkoani Guangxi: Harufu ya maua ya jasmine yaonesha hatua ya ustawishaji wa vijijini

“Miongoni mwa maua kumi ya Jasmine duniani, kuna 6 yaliyotoka huko Hengzhou.” Hivi sasa, maua ya Jasmine yamekuwa kadi inayojulikana sana ya mji mdogo huo wa Hengzhou, mkoani Guangxi. Eneo la mashamba ya kupandwa maua ya Jasmine la mji huo limezidi hekta 8000, wakulima wa maua wamekuwa zaidi ya laki 3.3, utoaji wa maua bichi ya Jasmine kwa mwaka ni zaidi ya tani elfu 95, na utoaji wa chai cha maua ya Jasmine kwa mwaka ni tani elfu 80, kila moja ya mbili hizi

inachukua zaidi ya 60% ya ile ya duniani. Thamani ya chapa ya bidhaa kwa ujumla imefika Yuan bilioni 21.53, ilichaguliwa tena kuwa chapa yenye thamani zaidi ya bidhaa za kilimo mkoani Guangxi.

Mkuu wa shamba la kielelezo alisema, mpaka sasa shamba hili limepanda maua ya Jasmine kwenye vyungu vya maua laki 3 kwa ujumla, hadi tarehe mosi, Julai, mwaka huu, shamba hili limeuza vyungu vya maua ya Jasmine laki 1.5 hivi, thamani ya uuzaji imefikia Yuan laki 7.5.

Kadiri maeneo ya shamba la kupandwa maua ya Jamine yanavyopanuka zaidi siku hadi siku, ndivyo mji wa Hengzhou unavyoweza kuongeza mapato ya wakulima kwa kupitia nguvu ya soko.

(Wahariri wa tovuti:Li Yidan,Zhao Jian)

Picha