Xi Jinping aendesha mkutano wa maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya Beijing 2022

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 15, 2021
Xi Jinping aendesha mkutano wa maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya Beijing 2022
(Picha zinatoka tovuti ya Shirika la Habari la China Xinhua.)

Mwanzoni mwa mwaka huu Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China ambaye pia ni rais wa China Xi Jinping alifanya ziara ya ukaguzi mjini Beijing na mkoani Hebei, na kuendesha Mkutano wa kusikiliza ripoti kuhusu maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi na Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi 2022, ambapo alitoa hotuba akisisitiza kuwa, kuandaa vizuri Michezo hiyo ya Olimpiki ni jambo kubwa kwa Chama na Taifa, ni ahadi tuliyotoa kwa umakini kwa jumuiya ya kimataifa, maandalizi ya michezo hiyo ni kazi ya fahari ambayo ina umuhimu mkubwa. Amesema China inatakiwa kuwa na nia thabiri, kufanya juhudi bila kuogopa taabu, kutekeleza wazo jipya la maendeleo, kufanya maandalizi bila ubadhirifu na ufisadi, kujitahidi kufanya vizuri maandalizi ya kazi zote, ili kuionesha dunia Michezo ya Olimpiki murua zaidi na ya kiwango cha juu.

Rais Xi alidhihirisha kuwa, kujenga nchi yenye nguvu ya kimichezo, ni lengo kubwa la kujenga nchi ya kisasa ya kijamaa. Msingi wa nchi yenye nguvu ya kimichezo ni kuwahamasisha wananchi washiriki kwenye michezo. Amesema China inatakiwa kusukuma mbele maendeleo ya michezo kwenye theluji na barafu, kuziba pengo, kupunguza udhaifu wa China kwenye michezo ya majira ya baridi, na kuhimiza michezo ya China iendelezwe kwenye kiwango cha juu katika zama mpya. Pia amesema wanamichezo wanapaswa kuongeza ujasiri na kufanya mazoezi bila kujali chochote, kuongeza uvumbuzi wa kiteknolojia, kujifunza na kuiga mawazo na teknolojia za kisasa kutoka kwa nchi nyingine, ili kuinua kiwango cha ushindani siku hadi siku. Rais Xi aliongeza kuwa, ni lazima kufuata wazo la kuandaa Michezo ya Olimpiki bila uchafuzi kwa mazingira, kufungamanisha maendeleo ya mambo ya michezo na ujenzi wa ustaarabu wa mazingira ya asili, kufanya zana na vifaa vya michezo vionekane katika hali ya kupatana na mandhari ya maumbile, na kuhakikisha watu wanaweza kujiburudisha katika michezo kwenye theluji na barafu yenye mvuto usio na kikomo. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha