Unaalikwa Kusherehekea Sikukuu ya Mwezi Pamoja Nasi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 17, 2021
Unaalikwa Kusherehekea Sikukuu ya Mwezi Pamoja Nasi

Sikukuu ya Tarehe 15 ya Mwezi wa 8 kwa kalenda ya kilimo ya China, kwa kawaida watu wengi wanaiita Sikukuu ya Mwezi, ambayo ni moja ya sikukuu kuu nne za jadi za China. Sikukuu hiyo ilianza kusherehekewa katika mwaka wa kwanza wa Enzi ya Tang, na imekuwa na historia ndefu.

Nchini China, mwezi mpevu unamaanisha kujumuika pamoja kwa watu wa familia moja moja, ndiyo maana sikukuu hiyo inaonesha hisia za watu za kukumbuka maskani, jamaa na marafiki, na kueleza matarajio juu ya mavuno na maisha ya furaha. Tarehe 15 ya Mwezi wa 8 kwa kalenda ya kilimo ya China ni Sikukuu ya Mwezi kila mwaka. Katika siku hiyo, watu hujistarehesha chini ya mwanga wa mwezi mpevu, na kula keki ya mwezi ya jadi.  (Picha zilipigwa na Li Yidan na Zhou Linjia.)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha