Wanaanga wa Shenzhou No.12 wafika Beijing salama

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 18, 2021
Wanaanga wa Shenzhou No.12 wafika Beijing salama
Septemba 17,jioni,Nei Haisheng(kati), Liu Boming(upande wa kulia), Yang Hongbo walipiga saluti.

Ofisi ya mradi wa kupeleka mtu kwenye anga ya juu ya China ilitoa habari zikisema, wanaanga Nei Haisheng, Liu Boming na Yang Hongbo ambao waliofanikisha chombo cha Shenzhou No. 12 cha kupeleka binadamu kwenye anga ya juu wamefika Beijing salama kwa kupanda ndege ya kikazi Septemba 17, 2021.

Mhusika alisema, baada ya kufikia Beijing kwa wanaanga hao watatu, wataingia kwenye kipindi cha kutengwa kwa ajili ya matibabu, na kupima afya na kupumzika.

Habari zilitolewa na Shirika la Habari la China Xinhua (Picha ilipigwa na Guo Zhongzheng) 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha