Katibu Mkuu wa UN atoa wito wa kuwa na mshikamano kwa moyo mmoja

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 18, 2021
Katibu Mkuu wa UN atoa wito wa kuwa na mshikamano kwa moyo mmoja
(Picha zinatolewa na UN.)

Tarehe 17, Septemba, 2021, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres aligonga kengele ya amani kwenye hafla ya Siku ya Amani ya Kimataifa iliyofanywa katika makao makuu ya UN huko New York. Alitoa wito wa kuwa na mshikamano kwa moyo mmoja wakati tarehe 21, Septemba, ambayo ni Siku ya Amani ya Kimataifa inapowadia.

Alisema, “sasa wakati umefika kwa kujenga upya dunia yetu, kuishi kwa mapatano na mazingira ya maumbile—na kuishi pamoja kwa amani na watu wengine, kuhimizana katika kujiendeleza badala ya kupambana, na kujenga siku nzuri za kweli za binadamu za baadaye.”

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha