Wanawake wa Tanzania waona mustakabali unaong’ara kwa kupitia upigaji picha (5)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 22, 2021
Wanawake wa Tanzania waona mustakabali unaong’ara kwa kupitia upigaji picha
(Picha zinatoka Tovuti ya Shirika la Habari la China Xinhua.)

Kijana Mwanamke anayetoka kitongoji cha jiji la Dar es Salaam, Bi.Lorraine Shose anatarajia kuchuma pesa nyingi baada ya kumaliza masomo yake ya kupiga picha.

Shose, aliye na umri wa miaka 28, alisema ameshiriki darasa la upigaji picha linalofanywa na Mpango wa Wapiga picha wa Wanawake (FPP), ambao unalenga kuwasaidia vijana na wanawake wadogo wajifunze upigaji picha ili kuongeza uwezo wake wa kiuchumi. Anaamini mustakabali wake unang’ara.

Bi.Shose ni mmojawapo wa wanawake 60 waliofundishwa na FPP kuhusu upigaji picha kuanzia mwaka 2020. Masomo hayo yanawawezesha wajipatia riziki kwa kupitia kupiga picha kwenye harusi na shughuli za michezo, utamaduni na kidini.

Fransisca Damian, mwanzilishi na kiongozi mtendaji wa LJF, alisema wingi wa vijana wanawake wanaofundishwa na FPP walifukuzwa shuleni kwa sababu ya mimba au ya kuwa mama asiye na mume.

Bi. Damian alisema, takwimu zinaonesha takribani asilimia 90 wa wapiga picha wa Tanzania ni wanaume.

Bi. Damian alisema, “upigaji wa picha unachochea ajira kwa vijana wanawake. Ninadhani wanawake hao ni watangulizi katika shughuli za upigaji picha na ni wanaobadilisha kanuni za michezo nchini Tanzania.” 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha