Wanasayansi wa China waunda wanga kwa kutumia dioksidi kaboni kwa mara ya kwanza

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 27, 2021
Wanasayansi wa China waunda wanga kwa kutumia dioksidi kaboni kwa mara ya kwanza
(Picha zinatoka Tovuti ya Shirika la Habari la China Xinhua.)

Wanasayansi wa China waligundua njia ya kuunda wanga kwa kutumia dioksidi kaboni, huu ni uvumbuzi wa kwanza duniani.

Utafiti huo umefanywa na Taasisi ya teknolojia ya biolojia ya viwanda ya Tianjin chini ya Taasisi ya Sayansi ya China, na tasnifu ya utafiti huo ilichapishwa kwenye jarida la "Sayansi" ("Science") ijumaa ya wiki iliyopita.

Mwanasayansi mmoja anayeshiriki utafiti huo alisema, muundo wa wanga huo ulioundwa na binadamu umethibitishwa kuwa ni sawasawa na muundo wa wanga asilia.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha