Maonyesho ya pili ya Uchumi na Biashara kati ya China na Afrika yafunguliwa kwenye sehemu ya kati ya China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 27, 2021
Maonyesho ya pili ya Uchumi na Biashara kati ya China na Afrika yafunguliwa kwenye sehemu ya kati ya China
(Picha zinatoka Tovuti ya Shirika la Habari la China Xinhua.)

Jumapili ya wiki iliyopita, Maonesho ya pili ya Uchumi na Biashara kati ya China na Afrika yamefunguliwa huko Changsha, mji mkuu wa mkoa wa Henan, katikati ya China.

Upande wa waandalizi ulisema, maonesho hayo yatafanywa kwa siku nne kwa njia ya video na kwenye ukumbi wa nyumba pia, na yamevutia kampuni karibu 900 kutoka nchi 40 hivi za Afrika na China.

Habari zinasema kuwa, matunda ya ushirikiano wa kiuchumi kati ya China na Afrika yataoneshwa kwenye maonesho hayo pamoja na bidhaa za chapa za Afrika, bidhaa zenye sifa ya kipekee kama vile kahawa, njugu n.k. Na pia itafanyika mijadala kuhusu ushirikiano kwenye sekta mbalimbali za chakula, mazao ya kilimo, matibabu na afya, mambo ya fedha, miundombinu na mashirika ya binafsi.

Maonesho hayo yalifanywa kwa mara ya kwanza mwaka 2019, ambayo ni jukwaa muhimu la kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na nchi za Afrika.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha