Tamasha la biashara ya mtandaoni lasaidia kuongeza mauzo ya bidhaa za Afrika nchini China (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 30, 2021
Tamasha la biashara ya mtandaoni lasaidia kuongeza mauzo ya bidhaa za Afrika nchini China

Kama sehemu ya shughuli zilizopangwa katika maonyesho ya pili ya uchumi na biashara ya China na Afrika ya mwaka 2021,tamasha la kuuza na kununua bidhaa mtandaoni lilifanyika tarehe 26 Septemba, siku ambayo maonyesho hayo ya uchumi na biashara yalifunguliwa katika mji wa Changsha, mkoani Hunan ambao kijiografia uko katikati nchini China.

Tamasha hilo ambalo ni la kwanza na la aina ya pekee ambalo linafanyika sambamba na maonyesho hayo, linalenga kujenga jukwaa la kuwezesha bidhaa za Afrika kuingia soko la China huku likipanua mtandao wa mauzo ya bidhaa. Katika kipindi cha siku tatu, zaidi ya shughuli 62 za biashara ya mtandaoni yalifanyika na majumba 10 kwa ajili ya shughuli hiyo vilitumika.

Waandaaji wa tamasha hilo waliarika watu wenye ushawishi mkubwa kwenye mtandao wa kijamii kutangaza bidhaa za Afrika. Bidhaa nyingi kati hizo ziliagizwa kutoka Afrika zikiwa ghafi na baadaye zilisindikwa, kufungashwa na kutangazwa na makampuni ya China na kasha kufikishwa sokoni.

Matangazo ya bidhaa yanatangazwa na makampuni kutoka vituo vya uhamasishaji biashara za mitandaoni kwenye kituo cha kielelezo cha utangazaji na ubunifu kilicho chini ya ushirikiano kati ya China na Afrika katika eneo la soko la Gaoqiao ambalo ni eneo pekee lenye maonyesho sambamba na yale makubwa yanayofanyika mji huo wa Changsha.

“Tumeshaandaa zaidi ya shughuli 4,200 za biashara ya mtandaoni tangu kuanzishwa kituo hiki, na thamani ya jumla ya mauzo yalifikia kiasi cha yuan milioni 550” alisema Mtendaji wa Soko la Gaoqiao la Changsha, ambaye aliongeza kwamba, tamasha hilo litasaidia kukusanya kwa pamoja rasilimali za bidhaa, majukwaa ya biashara za mtandaoni na njia za mauzo, ili kuwezesha kuleta faida kwa pande zote za China na Afrika. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha