Merkel afanya ziara ya mwisho Italia, akutana na Waziri Mkuu Draghi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 08, 2021
Merkel afanya ziara ya mwisho Italia, akutana na Waziri Mkuu Draghi
(Picha zinatoka Tovuti ya Shirika la Habari la China Xinhua.)

Waziri Mkuu wa Italia Mario Draghi Alhamisi ya wiki hii alimshukuru Chansela wa Ujerumani anayemaliza muda wake Angela Merkel kwa kubeba jukumu muhimu katika kujenga siku za baadaye za Umoja wa Ulaya (EU).

Kauli yake ameitoa wakati wa kuhitimishwa kwa ziara rasmi ya Merkel ambayo inaweza kuwa ya mwisho kukutana na viongozi wa juu wa Italia, kutokana na kujiandaa kuachia madaraka hivi karibuni wakati Serikali ya Shirikisho la Ujerumani itakapoundwa kufuatia kufanyika kwa uchaguzi wa kibunge hivi karibuni.

“Namshukuru Chansela kwa niaba ya Serikali na mimi binafsi kwa jukumu mahsusi la kubuni baadaye ya Ulaya kwa zaidi ya miaka 16 iliyopita” alisema Draghi kwenye mkutano wa pamoja na waandishi wa habari.

Kwa upande wake, Merkel alisema kwamba Draghi ametoa na mchango muhimu katika kuilinda sarafu ya euro.

“Naamini euro inawakilisha umoja wetu (EU), kwahiyo juhudi zaidi inabidi ziongezwe katika kuiimarisha na kuiendeleza….na kuna mengi zaidi yanayohitaji kufanywa katika eneo hili” alisema.

Mazungumzo kati ya Merkel na Draghi yaligusia masuala mengine kama vile malengo ya G20 ambayo kwa sasa nchi mwenyekiti wa zamu ni Italia , haja ya kuongeza usambazaji wa chanjo dhidi ya UVIKO-19 duniani, na hali ilivyo nchini Afghanistan ambao Ujerumani na Italia zilikuwa na msimamo mmoja.

Viongozi hao wawili pia walizungumzia mabadiliko ya hali ya hewa na uhifadhi wa mazingira kwa kurejea Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Hali ya Hewa (COP26) ambao unatarajiwa kufanyika Glasgow, Uingereza kati ya Oktoba 31 na Novemba 12 mwaka huu. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha