UNHCR yataka ksimamisha kukamata watafuta hifadhi nchini Libya (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 09, 2021
UNHCR yataka ksimamisha kukamata watafuta hifadhi nchini Libya

Kamishna Mkuu wa Shirika la kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) Ijumaa ya wiki hii ametaka kusimamisha kukamata watu wanaotafuta hifadhi nchini Libya, akihimiza kuanzisha tena ndege za kuwasafirisha watu wanaotafuta hifadhi na wakimbizi kwenda nchi za nje.

 "Tunaendelea kutoa wito kwa mamlaka: kuheshimu wakati wote haki za binadamu za wanaotafuta hifadhi na wakimbizi, kusimamisha kukamatwa kwao, na kuwaachilia huru wale waliokamatwa, pamoja na wale ambao walitaka kuondoka kwa safari za ndege ," taarifa iliyotolewa na UNHCR ilisema.

 "Tunatoa ombi letu tena kwa mamlaka za Libya kuruhusu kuanza tena kwa safari za ndege za kibinadamu kuondoka nje ya nchi, ambazo zimesimamishwa kwa karibu mwaka mmoja," iliongeza.

 UNHCR ilielezea wasiwasi juu ya hali ya kibinadamu ya watafut hifadhi na wakimbizi nchini Libya, kufuatia kukamatwa na shambulizi dhidi yao unaoendelea katika maeneo mengi ya mji mkuu Tripoli baada ya operesheni kubwa ya usalama iliyoendeshwa na mamlaka ya Libya katika wiki iliyopita.

 Angalau mtu mmoja aliripotiwa kuuawa, 15 walijeruhiwa, na zaidi ya watu 5,000 wamekamatwa na kushikiliwa katika vituo kadhaa vya kizuizini vyenyehali ya msongamano mkubwa na hali mbaya ya usafi, ilisema taarifa hiyo.

 Kamishna huyo pia alisema shambulizi hilo, ambalo pia lilihusisha ubomoaji wa majengo mengi ambayo hayajakamilika na nyumba za muda, umesababisha wasiwasi na hofu miongoni mwa wanaotafuta hifadhi na wakimbizi mjini Tripoli, wakiwemo watoto wasio na wazazi na wakina mama wenye watoto wachanga.

Libya imekuwa ikikumbwa na ukosefu wa usalama na machafuko tangu kiongozi aliyefariki Muammar Gaddafi kuondolewa madarakani mnamo 2011, na kuifanya nchi hiyo kuwa mahali pa kupendwa ya wahamiaji haramu ambao wanataka kuvuka Bahari ya Mediterranean kwenda Ulaya.

Wahamiaji waliookolewa wanaishi katika vituo vya mapokezi vinavyojaa watu kote nchini Libya, licha ya wito wa mara kwa mara wa kimataifa wa kufunga vituo hivyo. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)

Picha