Eneo la Dunhuang lenye utamaduni wa historia ndefu la kuwepo pamoja na milima na chemchemi (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 11, 2021
Eneo la Dunhuang lenye utamaduni wa historia ndefu la kuwepo pamoja na milima na chemchemi

Katika historia, eneo la Dunhuang lilikuwa kama koo la Njia ya Hariri ya kale, na ni eneo muhimu la kijeshi. Watu wakifika Dunhuang, hakika watatembelea Pango la Mogao. Pango la Mogao liliitwa “ Pango la Buddha elfu moja” ambalo liko kwenye miamba ya kando ya magharibi ya Mto Dangquan na mashariki ya sehemu ya chini ya Milima Mingsha, kilomita 25 kutoka kusini mashariki mwa mji wa Dunhuang wa mkoa wa Gansu, urefu wa pango hilo ni mita 1680. Likiwa moja kati ya mapango makubwa manne maarufu ya China, Pango la Mogao lilichimbuliwa kuanzia mwaka wa 366, mpaka sasa limekuwa na historia ya miaka 1655. Mwaka 1987 ilichaguliwa kuwa urithi wa utamaduni wa dunia wa China kwa mara ya kwanza, pango hilo ni mabaki ya sanaa ya dini ya Kibudha yenye eneo kubwa zaidi, historia ndefu zaidi, linalohusu mambo mengi zaidi na lenye sanaa murua zaidi duniani.

Milima Mingsha iliundwa na mchanga uliohama kwa kufuata maji yaliyotiririka, ambapo mchanga ulipohama uliweza kutoa mlio hivyo milima ilipata jina la Mingsha, Ming, maana yake ya Kichina ni kutoa sauti, Sha, maana yake ya Kichina ni mchanga. Mchanga mdogomdogo una rangi tano za nyekundu, manjaro, kijani, nyeusi na nyeupe. Katikati ya Milima Mingsha kuna chemchemi moja inayoitwa Chemchemi ya Mwezi, kwa sababu umbo lake linafanana na mwezi mpevu. (Mwandishi wa habari wa tovuti ya gazeti la umma:Zhao Guangxia) 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)

Picha