Mashindano ya Kimataifa ya Masimulizi ya Hadithi ya “Majaaliwa na Lugha ya Kichina” ya 2021 yamalizika (9)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 13, 2021
Mashindano ya Kimataifa ya Masimulizi ya Hadithi ya “Majaaliwa na Lugha ya Kichina” ya 2021 yamalizika

Oktoba 12- Habari kutoka kwenye Tovuti ya Gazeti la Umma ya Xining (mwandishi wa habari: Ai Wen) Mashindano ya Kimataifa ya Masimulizi ya Hadithi ya “Majaaliwa na Lugha ya Kichina” ya mwaka 2021 yaliyoandaliwa na Shirika la Urafiki wa Watu wa China kwa watu wa Nchi za nje, ambayo yaliendeshwa na Tovuti ya Gazeti la Umma na Serikali ya mji wa Xining yamemalizika tarehe 12 Oktoba huko Xining, mkoa wa Qinghai.

Washiriki 10 wa mashindano hayo kutoka Ujerumani, Kazakhstan, Argentina, India, Japani, Syria, Ufaransa, Zimbabwe, Jamhuri ya Kongo na Marekani kila mmoja alitoa maelezo yake ya dakika 7 yenye maudhui ya neno la Kichina ‘Ren’, maana yake ni moyo mwema .

Waamuzi waliwapa alama kutokana na uwezo wa masimulizi waliyotoa kwa Kichina, mvuto wao kwa wasikilizaji kwenye mashindano, na mtazamo wao kuhusu maadili makuu katika masimulizi yao ya hadithi. Hatimaye, Yang Jing kutoka Zimbabwe alikuwa mshindi wa kupata tuzo maalum; Ma Li (Syria), Jingjing (Kazakhstan) walishinda tuzo ya nafasi ya kwanza; Xiaoyu (India, miaka 10), Li Hongyu (Argentina), na Ai Jie (USA) walipata tuzo ya nafasi ya pili; Tanishita Mari (Japan), Charles (Jamhuri ya Kongo), Richard (Ufaransa) na Christoph (Ujerumani) walipata tuzo ya nafasi ya tatu.

Bw. Li Xikui, naibu mkurugenzi wa Shirika la Urafiki wa Watu wa China kwa watu wa Nchi za nje alitoa risala akisema, kuchagua neno “Ren” la Kichina kama maudhui ya masimulizi ya hadithi kwenye mashindano hayo ya kimataifa, kunalenga kuwafanya marafiki wengi zaidi waelewe mawazo ya Taifa la China kuhusu amani, maafikiano na masikilizano. Hivi sasa maambukizi ya virusi vya Corona bado yanaenea duniani kote, dunia inahitaji nguvu ya kiroho ya “Renai”, maana yake ya Kichina ni wema na upendo, na wanatakiwa kushirikiana katika kujenga jumuiya ya binadamu ya mustakabali wa pamoja.

Tangu mashindano hayo ya kimataifa ya masimulizi ya hadithi yalipoanzishwa Mei 17, yaliitikiwa na mashabiki zaidi ya 3000 wa masomo ya lugha ya Kichina kutoka nchi na sehemu zaidi ya 50 za nchini na ng’ambo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)

Picha