China yaanzisha hifadhi za taifa za kwanza kwenye mikoa 10 (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 14, 2021
China yaanzisha hifadhi za taifa za kwanza kwenye mikoa 10
Hifadhi ya taifa ya chanzo cha mito mitatu

Oktoba 13-Habari kutoka Kunming mkoani Yunnan zinasema, Hifadhi za taifa zinathibitishswa na kusimamiwa na serikali kuu, haya ni mambo muhimu ya ujenzi wa utaratibu kuhusu uhifadhi wa hali ya viumbe. Oktoba 12 kwenye mkutano wa kilele wa mkutano wa 15 wa nchi zilizosaini Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Anuwai ya Viumbe , orodha ya hifadhi za taifa za kwanza za China zimetangazwa.

Hifadhi ya taifa ya chanzo cha mito mitatu, hifadhi ya taifa ya Panda, hifadhi ya taifa ya tiger na chui wa kaskazini mashariki, hifadhi ya taifa ya msitu wa mvua ya kitropiki ya Hainan na hifadhi ya taifa ya Mlima Wuyi zimekuwa hifadhi za taifa za kwanza zilizoanzishwa rasmi na serikali ya China, hifadhi hizo zimeanzishwa katika mikoa 10 ya Qinghai, Tibet, Sichuan, Shaanxi, Gansu, Jilin, Heilongjiang, Hainan, Fujian, Jiangxi, mikoa hiyo yote iko kwenye maeneo muhimu ya muundo wa kimkakati wa usalama wa hali ya viumbe wa nchi yetu, na maeneo ya hifadhi yalifikia kilomita 230,000 za mraba, na kuhusisha karibu 30% ya aina za wanyamapori na mimeapori ambazo zinawekwa mkazo na serikali katika kuhifadhiwa.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)

Picha