Maonesho ya urithi wa kitamaduni usioshikika yafunguliwa Xinjiang, China (5)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 19, 2021
Maonesho ya urithi wa kitamaduni usioshikika yafunguliwa Xinjiang, China
Jumba la Maonesho wa Aksu, eneo la Xinjiang (Picha za Tovuti ya Gazeti la Umma/Han Ting)

Maonesho ya urithi wa kitamaduni usiyoshikika yameanza Jumanne ya wiki iliyopita, kwenye Jumba la makumbusho la Sanaa la Xinjiang huko Urumqi, mji mkuu wa Mkoa unaojiendesha wa Xinjiang unaopatikana Kaskazini Magharibi mwa China.

Maonesho hayo ya siku sita yanatarajiwa kuonesha kazi bora 209 za urithi wa kitamaduni usiyoshikika kutoka mikoa na miji 19 ambayo umetoa msaada kwa ujenzi wa Xinjiang, pamoja na miji na maeneo 14 katika mkoa huo.

Hafla hiyo pia inahusisha "maonesho ya mtandaoni" na shughuli za nje ya mtandao. Karibu wawakilishi 100 wa urithi wa kitamaduni usiyoshikika pia wamealikwa kwenye hafla hiyo.

Maonesho hayo yameandaliwa kwa pamoja na Wizara ya Utamaduni na Utalii ya China na Serikali ya Xinjiang.

Hadi sasa, Xinjiang ina urithi wa kitamaduni usiyoshikika wa aina tatu kwenye orodha ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), 94 kwenye orodha ya kitaifa, na 315 kwenye orodha ya mkoa huo unaojiendesha. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha