Mkutano ujao wa FOCAC kukuza uhusiano kati ya China na Afrika katika sekta mbali mbali: Mtaalam wa Ethiopia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 19, 2021
Mkutano ujao wa FOCAC kukuza uhusiano kati ya China na Afrika katika sekta mbali mbali: Mtaalam wa Ethiopia
Picha iliyopigwa Septemba 14, 2021 ikimuonesha Getachew Adem Tahir, Naibu Kamishna wa zamani wa Tume ya Mipango ya Kitaifa ya Ethiopia, huko Addis Ababa, Ethiopia. (Xinhua / Michael Tewelde)

ADDIS ABABA - Mkutano ujao wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) utakuza uhusiano kati ya pande hizo mbili katika sekta mbalimbali za kijamii, kiuchumi na kisiasa, mtaalam wa mipango ya maendeleo amesema.

Katika mahojiano ya hivi karibuni na Shirika la Habari la China, Xinhua, Getachew Adem Tahir, Naibu Kamishna wa zamani wa Tume ya Mipango ya Kitaifa ya Ethiopia, amesema viongozi wa Afrika na China wanatazamiwa kuimarisha zaidi maendeleo yaliyopo na ushirikiano wa kisiasa wakati wa mkutano wa FOCAC, ambao umepangwa kufanyika nchini Senegal baadaye mwaka huu.

Kwa mujibu wa mtaalam huyo, mkutano huo utaleta matokeo dhahiri katika kufufua uchumi wa nchi za Afrika ambao umeathiriwa na janga la UVIKO-19 linaloendelea pia kuimarisha uhusiano wa China na Afrika katika maeneo tofauti ya ushirikiano.

"Ninaamini, viongozi wa Afrika na China watazungumza masuala ya namna ya kushughulikia athari za janga la UVIKO-19 kwani suala la maendeleo ni muhimu sana," mtaalam huyo amesema.

Huku akizingatia kwamba nchi zinazoendelea barani Afrika na kwingineko duniani kwa sasa zinakabiliwa na changamoto katika kupata chanjo ya UVIKO-19, mtaalam huyo alisisitiza kuwa kupatikaka kwa urahisi wa chanjo ya UVIKO-19 itakuwa ni ajenda muhimu kwa viongozi hao wakati wa mkutano huo.

 "Kwa upande wa kisiasa, nchi za Afrika zinakabiliwa na changamoto za usalama kama vile uwepo wa mizozo na matukio ya kigaidi. Kwa maana hiyo, jinsi gani nchi zinaweza kutatua changamoto hizi ni suala lingine litakaloshughulikiwa na viongozi hao” Tahir amesema.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha