Matokeo mapya mengi yaonekana kwenye Mkutano wa Mtandao wa Intaneti wa Viwanda wa Dunia 2021

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 20, 2021
Matokeo mapya mengi yaonekana kwenye Mkutano wa Mtandao wa Intaneti wa Viwanda wa Dunia 2021
Mkutano wa Mtandao wa Intaneti wa Viwanda wa Dunia wa 2021 ulifanyika tarehe 18 hadi 19 mjini Shenyang, Liaoning. Mpiga picha:Sun Boyang

Maonesho ya matokeo mapya ya Mkutano wa Mtandao wa Intaneti wa Viwanda wa Dunia 2021 yamefanyika mjini Shen Yang kuanzia Tarehe 18 hadi 20, Oktoba, ambayo yamevutia washiriki wa kampuni maarufu karibu 120 za nchini na ng’ambo zinazohusika na sekta ya mtandao wa intaneti wa viwanda na viwanda husika vya utengenezaji.

Habari zilisema, maonesho hayo yanagawanywa kwenye maeneo saba yenye mita elfu 20 za mraba, ambapo kuna maonesho ya matokeo ya kitaifa na mkoa wa Liaoning, yanayohusisha sekta tatu za mtandao wa intaneti wa viwanda, jukwaa na usalama husika.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha