Mfano wa China katika ulinzi wa baioanuai unastahili kuigwa: mtetezi wa uhifadhi wa Sri Lanka

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 21, 2021

COLOMBO - Miongozo ya China juu ya uwekezaji wa kimataifa na msisitizo wake wa ndani juu ya maendeleo yasiyo na uchafuzi wa mazingira ni kati ya mambo ambayo Sri Lanka na Dunia inastahili kujifunza, kiongozi wa kibiashara na mtetezi wa uhifadhi mazingira kutoka Sri Lanka amesema

Dilhan Fernando, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Dilmah Tea na Mkurugenzi wa Uhifadhi wa Dilmah, ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua kwamba mazungumzo ya mikutano ya kimataifa ya COP yamekuwa yakipata maendeleo polepole na yameshindwa kutoa ushirikiano unaohitajika ili kupiga hatua zaidi.

Kinyume chake, mkutano wa 15 wa pande zilizotia saini Mkataba wa Umoja wa Mataifa juu ya Baioanuai (COP15) uliofanyika hivi karibuni huko Kunming, China umezileta nchi pamoja juu ya suala hili, hivyo italeta mabadiliko.

"Azimio la Kunming lenye ujasiri na mambo ya rasmi ndilo tunapaswa tuipongeze China" Fernando ameongeza.

"Fursa katika karne hii zimeendana zaidi na uchumi usiosababisha uchafuzi wa mazingira. Kwa maana hiyo, ukiangalia bioanuwai, sio kuhusu uhifadhi wa mazingira ya asili, bali inahusu kuhifadhi rasilimali kwa ajili ya maendeleo endelevu," ameelezea.

Fernando amekumbusha kwamba dunia imepuuza Maoni ya Stern juu ya uchumi wa maabadiliko ya tabianchi, ripoti ambayo iliyotolewa na Mwanauchumi Nicholas Stern mwaka 2006, Mwenyekiti wa taasisi ya utafiti juu ya masuala ya mabadiliko ya tabianchi na mazingira ya Grantham, katika chuo cha Uchumi cha London.

Lakini azimio la Kunming litakuwa la tofauti kwa kuwa, katika mkutano wa mwaka huu wa COP15 wa Kunming, makubaliano yamefikiwa kati ya washiriki wa Jopo la Kimataifa juu ya Mabadiliko ya Tabianchi "kwa malengo yaliyo wazi, halisi na yanayopimika."

Fernando ameendelea kusema kuwa utekelezaji wa malengo ya hali ya hewa hauwezi kufanywa na serikali pekee na kwamba wafanyabiashara na watu binafsi pia wanapaswa kubadilisha tabia zao. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha