Kauli ya Marekani kuhusu maabara ya Wuhan unatokana na siasa ya kijiografia: Gazeti la Pakistan

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 21, 2021

ISLAMABAD – Gazeti la Kiingereza la kila siku la Pakistan "The Express Tribune" linasema, kauli ya Marekani kuhusu maabara ya Wuhan ya China haitokani na sayansi bali siasa ya kijiografia, ikiwa na lengo mahsusi la kuichafua China na watu wake, limeripoti.

Uongo wa Marekani una nia ya wazi ya kuwafanya wachina kuwajibika na janga la UVIKO-19, gazeti hilo limenukuu makala iliyochapishwa Jumamosi iliyopita na tovuti ya Soshalisti Duniani.

Makala hiyo iliyopewa jina la "Uongo kuhusu Maabara ya Wuhan: Washington Post inafundisha Chuki Wamarekani" imekosoa tahariri mpya ya gazeti la The Washington Post, ambayo imehuisha madai yaliyokataliwa kwamba UVIKO-19 umetokana na virusi vilivyobuniwa watafiti wa China, gazeti hilo la Pakistan limesema.

Gazeti hilo limesema kuwa, kila neno na madai ambayo yamechapishwa kwenye gazeti la "The Washington Post" yamekuwa yakikanushwa mara kwa mara na wanasayansi, mashirika ya kimataifa na hata serikali ya Marekani yenyewe.

Mapema mwaka huu, uchunguzi juu ya chimbuko la UVIKO-19 uliofanywa na wataalam wa Shirika la Afya Duniani (WHO) ulibainisha kuwa kauli kuhusu virusi vya korona kuvuja kutoka maabara kwa kiwango kikubwa haiwezekani, lakini Washington Post linapuuza matokeo hayo kwa makusudi.

Gazeti hilo linasema, makala yaliyochapishwa kwenye "The Washington Post" kinaonekana kimeandaliwa kwa uangalifu na kuratibiwa na idara ya upelelezi ya Marekani, kama haijaandikwa moja kwa moja na gazeti hilo, gazeti la "The Washington Post" ni chombo cha ubeberu wa Marekani.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha