Ingia Kwenye Hifadhi ya Tiger wa Kaskazini Mashariki Hisi Mvuto wa Mfalme wa Msituni (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 26, 2021
Ingia Kwenye Hifadhi ya Tiger wa Kaskazini Mashariki Hisi Mvuto wa Mfalme wa Msituni
Mfugaji aliwalisha watoto wa tiger katika hifadhi hiyo. Mpiga picha: Su Jinggang/Tovuti ya Gazeti la Umma

Tovuti ya Gazeti la Umma limeleta habari kutoka Mudangjiang Oktoba 25, kuwa Hifadhi ya tiger wa kaskazini mashariki ya Hengdaohezi amabyo iko mji wa Hailin wa Mudanjiang wa mkoa wa Heilongjiang ni kituo kikubwa zaidi duniani cha kufuga tiger wa Siberia na huitwa “maskani ya tiger ya China”. Juzijuzi waandishi wa habari waliingia huko na kufahamishwa kuwa tangu kuanzishwa kwa kituo hicho mwaka 1986, idadi ya tiger wa kaskazini mashariki imekuwa zaidi ya elfu moja kutoka 12 ya awali katika kituo hicho cha kufuga tiger wa aina hii.

Hifadhi hiyo inazungukwa na milima, eneo lake linalofunikwa kwa misitu linafikia asilimia 98, ambalo linafanana zaidi na mazingira ya asili ya ukuaji wa tiger wa kaskazini mashariki, na linasaidia tiger wa kaskazini mashariki wazoee hali ya porini na kuongeza uwezo wao wa kuishi porini, ili kuweka msingi wa kuwawezesha warudi kwenye mazingira ya asili hatimaye.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)

Picha