Rais Xi Jinping wa China atoa wito wa kujenga nguvu ya China katika sayansi na teknolojia

(CRI Online) Oktoba 27, 2021
Rais Xi Jinping wa China atoa wito wa kujenga nguvu ya China katika sayansi na teknolojia
(Picha zinatoka tovuti ya Shirika la Habari la China Xinhua.)

Rais Xi Jinping wa China amewataka wanasayansi na wanateknolojia nchini waendelee kujitahidi kujenga nguvu za China katika nyanja za sayansi na teknolojia.

Rais Xi amesema hayo alipotembelea maonyesho ya mafanikio ya China katika uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia katika kipindi cha Mpango wa 13 wa Miaka Mitano ya Maendeleo ya Jamii na Uchumi (2016-2020) mjini Beijing.

Rais Xi alidhihirisha kuwa, katika kipindi hicho cha kutekeleza Mpango wa 13 wa miaka mitano, sekta ya sayansi na teknolojia imepata maendeleo ya kasi, uwezo wa kufanya uvumbuzi umeinuka sana, China imepata mafanikio makubwa ya kisayansi na kiteknolojia katika nyanja za msingi, teknolojia ya hali ya juu ya kimkakati, na sayansi na teknolojia kuhusu maisha ya watu. Wakati China ikianza safari mpya ya kujenga nchi ya kijamaa ya kisasa katika nyanja zote, uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia utakuwa na nafasi kubwa muhimu katika kukuza maendeleo ya mambo ya jumla ya Chama na nchi. Alisema, wafanyakazi wa sekta ya sayansi na teknolojia wanatakiwa kufanya juhudi zaidi katika nyanja za teknolojia ya hali ya juu, ujenzi wa uchumi wa nchi, kukidhi mahitaji makubwa ya nchi, kuinua kiwango cha afya ya watu, kushika kithabiti nafasi za kufanya uvumbuzi, ili kutoa mchango mkubwa zaidi kwa ajili ya kuijenga China iwe nchi yenye nguvu kwenye nyanja za sayansi na teknolojia duniani, na kutimiza ustawishaji mkubwa wa Taifa la China.

Maonyesho hayo yameshirikisha zaidi ya vifaa na mifano 1,500. Miongoni mwao ni chombo cha uchunguzi wa Mwezi cha Chang'e-5, kigari cha kuchunguza Mars, sampuli ya kompyuta ya quantum Jiuzhang, na nyambizi ya Fendouzhe.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha