Medali za Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi na Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi ya Beijing 2022 Zatolewa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 27, 2021
Medali za Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi na Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi ya Beijing 2022 Zatolewa
Shughuli ya wakati wa siku 100 zinazobaki kabla ya Michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi ya Beijing ya mwaka 2022 ilifanyika kwa shangwe Beijing tarehe 26, Oktoba. Mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama, ambaye pia ni naibu waziri mkuu wa China na kiongozi wa kikundi cha uongozi wa kazi ya Michezo ya Olimpiki ya 24 ya majira ya baridi Bw. Han Zheng alishiriki kwenye shughuli hiyo, na kutangaza kutolewa kwa medali za Michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi ya Beijing “Tongxin” ambayo maana yake ya Kichina ni “kushirikiana kwa moyo mmoja ”.

Medali ya “Tongxin” ya Michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi ya Beijing inasanifiwa kuwa na michoro ya maduara manne na duara moja halisi katikati, kwa jumla ni maduara matano, ambayo yanamaanisha kuwa na moyo mmoja, na kueleza mawazo ya falsafa ya jadi ya China “mbingu, ardhi na binadamu kuishi pamoja kwa masikilizano” , pia inaashiria Moyo wa Olimpiki unawaunganisha watu pamoja.

Usanifu wa medali za Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya majira ya baridi unafanana na ule wa medali ya Michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi, ambayo inaonesha michoro ya maduara manne na duara moja halisi katikati , lakini sehemu ya katikati ya mbele ya medali imechongwa nembo ya Kamati ya Kimataifa ya Michezo ya Olimpiki ya Walemavu.  

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha