

Lugha Nyingine
Mahali palipokuwa eneo la Kiwanda cha Chuma cha Mji Mkuu Beijing pamekuwa Bustani ya Michezo ya Olimpiki (2)
Tarehe 26, Oktaba, wakati zimebaki siku 100 kabla ya Michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi ya Beijing, Bustani ya Michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi ya Beijing yalifunguliwa rasmi. Mjini Beijing kutafanyika kwa michezo miwili ya Olimpiki, sasa kumekuwa na bustani mbili za Michezo ya Olimpiki—Bustani ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing na Bustani ya Michezo ya Olimpiki ya Beijing, ambazo zinatia rangi nzuri kwa Beijing.
Chini ya jitihada za pande mbalimbali, “Bustani ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing” imejengwa kwenye eneo la Bustani ya Shougang. Tarehe 4, Januari, mwaka huu, Kamati ya Michezo ya Olimpiki ya kimataifa (IOC) iliidhinisha kutumia jina lake. Eneo la bustani hiyo kwa jumla lina hekta 171.2, pamoja na jukwaa kuu la urukaji kwenye michezo ya kuteleza juu ya theluji la Shougang, makao makuu ya Kamati ya Maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya Beijing, Kituo cha uendeshaji wa Michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi ya Beijing pamoja na vituo vingine vya uendeshaji wa michezo mbalimbali.
Likipita miaka 100 na Michezo miwili ya Olimpiki, Kundi la Shougang, yaani Kiwanda cha Chuma cha Mji Mkuu Beijing cha zamani kilifanyiwa mageuzi katika wakati wa Michezo ya Olimpiki ya Beijing 2008, na kujenga upya sura yake katika wakati wa Michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi ya Beijing 2022, ambapo eneo lililokuwa la kiwanda hicho limejengwa kuwa eneo la maendeleo mapya la kufanyia michezo, kufanya mazoezi ya kujenga mwili na kufanya shughuli za burudani, linaendelea sambamba na Michezo ya Olimpiki na kustawi kwa kufuata zama tulizonazo.
Kamati ya michezo ya Olimpiki ya Kimataifa ilisema, Bustani ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Bejing itakuwa moja kati ya mali kubwa zaidi za urithi wa michezo hiyo. Eneo lililokuwa la kiwanda cha chuma cha mji mkuu Beijing limekuwa eneo la mfano wa kuigwa wa kurekebisha muundo wa shughuli na kulinda mazingira.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma