Rais Xi ahimiza hatua madhubuti kushughulikia mabadiliko ya tabianchi, na masuala ya nishati

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 01, 2021
Rais Xi ahimiza hatua madhubuti kushughulikia mabadiliko ya tabianchi, na masuala ya nishati
Picha 1: Rais Xi Jinping wa China akihudhuria Mkutano wa 16 wa Viongozi wa G20 kwa njia ya video mjini Beijing, Mji Mkuu wa China, Oktoba 31, 2021. (Xinhua/Li Xueren)

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping siku ya Jumapili ya wiki iliyoisha ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua madhubuti kushughulikia mabadiliko ya tabianchi na masuala ya nishati.

Xi ameyasema hayo alipokuwa akihutubia kwenye Mkutano wa 16 wa Viongozi wa nchi wanachama 20 zenye uchumi mkubwa zaidi duniani (G20) unaofanyika Rome, Italia.

Xi amesema kwamba, mabadiliko ya tabianchi na masuala ya nishati ni changamoto kuu za dunia ya leo, ambazo zinahusu maslahi ya pamoja ya jumuiya ya kimataifa na mustakabali wa Dunia.

Nia na motisha ya jumuiya ya kimataifa kufanya kazi kwa pamoja ili kukabiliana na changamoto inaendelea kuongezeka, na muhimu ni kuchukua hatua madhubuti, amesema.

Ametoa wito kwa dunia kupitisha sera za kina na zenye uwiano, na kusawazisha ulinzi wa mazingira na maendeleo ya kiuchumi, pamoja na kushughulikia mabadiliko ya tabianchi na kulinda maisha ya watu. Nchi zenye uchumi mkubwa zinapaswa kuimarisha ushirikiano katika eneo hili, ameongeza.

Xi amesisitiza juu ya haja ya utekelezaji kikamilifu na kwa ufanisi Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya tabianchi na Makubaliano ya Paris, kuzingatia jukumu la Umoja wa Mataifa (UN) kama njia kuu, kufuata kanuni ya uwajibikaji wa pamoja lakini wenye kutofautisha majukumu, kufuata sheria za kimataifa, na kuwa na mwelekeo wa vitendo.

Pia amesisitiza umuhimu wa kuchukua hatua kali na kuimarisha ushirikiano.

Rais huyo wa China pia amezitaka nchi zilizoendelea kuongeza uungaji mkono wao kwa nchi zinazoendelea, akisema kuwa wanachama wa G20 wanapaswa kuongoza katika kukuza na kutumia teknolojia ya hali ya juu, na nchi zilizoendelea zinapaswa kutimiza kwa dhati ahadi zao kwa nchi zinazoendelea katika kutoa fedha za kusaidia kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Katika miaka 15 iliyopita, China imevuka lengo ililokuwa imejiwekea la kupunguza utoaji wa kaboni ifikapo Mwaka 2020, Xi amesema.

Ameongeza kwamba, China itaendelea kuhimiza mabadiliko na uboreshaji wa mundo wa nishati na viwanda, kuhimiza utafiti, maendeleo na matumizi ya teknolojia ya kijani na yenye kuzalisha kaboni kidogo, kuunga mkono maeneo yenye sifa, viwanda na makampuni ya biashara ili kuongoza katika kupunguza utoaji wa kaboni, na kutoa mchango katika juhudi za kimataifa za kushughulikia mabadiliko ya tabianchi na kukuza mabadiliko ya nishati, Xi amesema.

Kwa sasa, kuenea kwa janga la virusi vya korona kumesababisha migogoro mingi, Xi amesema, huku akiongeza kuwa mafanikio ya maendeleo yaliyopatikana katika jumuiya ya kimataifa kwa miaka mingi yamemomonyoka na nchi zinazoendelea zinakabiliwa na changamoto na majaribio ambayo hayajawahi kushuhudiwa.

Janga la UVIKO-19 kwa mara nyingine tena limeonesha kuwa, nchi zote zenye umuhimu mkubwa katika mustakabali wa pamoja na zenye maslahi yanayoingiliana na kuhusiana moja kwa moja, na huunda jumuiya yenye mustakabali wa pamoja, Xi amesema, huku akidhihirisha kwamba kukuza maendeleo endelevu katika nchi zinazoendelea kutanufaisha watu wa nchi husika, na pia kusaidia mustakabali wa wanadamu wote na Dunia.

Hivi karibuni China imezindua Mpango wa Maendeleo ya Dunia na kuitaka jumuiya ya kimataifa kuharakisha utekelezaji wa Ajenda ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo Endelevu ya 2030 na kuhimiza maendeleo yenye nguvu zaidi ya kijani kibichi na yenye afya kwa Dunia, na kuongeza kuwa nchi wanachama wa G20 zinapaswa kujenga maelewano na kuongeza kasi ya kutenda zaidi katika suala hili.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha