Maua ya chrysanthemum yanayochanua yawa maua ya kuleta mapato zaidi kwa wakulima wa Baokang, (5)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 03, 2021
 Maua ya chrysanthemum yanayochanua yawa maua ya kuleta mapato zaidi kwa wakulima wa Baokang,

Oktoba 25,2021,katika siku nzuri ya hali ya hewa, wakulima wa wilaya ya Baokang ya mji wa Xiangyang mkoani Hubei walichuma, kuchagua, na kuoka maua ya chrysanthemum katika hali ya pilikapilika .

Katika miaka ya hivi iliyopita, wilaya ya Baokang ikitegemea eneo lake lenye hali nzuri kijioglafia na hali ya hewa inayofaa imeendeleza upandaji wa maua ya chrysanthemum ambayo ni maua mazuri na yenye thamani ya juu ya kiuchumi, na kuongoza viwanda kutengeneza kwa kina bidhaa za maua ya chrysanthemum ili kupata nyongeza za thamani ya maua hayo, kuwasaidia wanakijiji wapate mapato zaidi, na kuhimiza kilimo na shughuli za utalii za huko ziende sambamba. Mpiga picha: Yang Tao(Tovuti ya Picha za Umma)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha