Uvunaji wa pamba kwa kutumia mashine waleta ufanisi na mapato zaidi kwa mkulima wa pamba wa Xinjiang (8)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 05, 2021
Uvunaji wa pamba kwa kutumia mashine waleta ufanisi na mapato zaidi kwa mkulima wa pamba wa Xinjiang
Amar Aziz (Kulia) akizungumza na rafiki yake katika shamba lake la pamba katika Mji wa Gezkum wa Kaunti ya Xayar, eneo la Aksu la Mkoa unaojiendesha wa Xinjiang nchini China, Oktoba 25, 2021. (Xinhua/Ma Kai)

Amar Aziz anaishi katika Kaunti ya Xayar, eneo la Aksu, ambayo ni eneo muhimu la kuzalisha pamba huko Xinjiang. Familia yake imekuwa ikipanda pamba kwa zaidi ya miaka 20. Katika miaka iliyopita, upandaji na uvunaji wa pamba ulitegemea nguvukazi. Katika msimu wa kuchuma pamba, huku wachumaji pamba zaidi ya kumi wakiwa wameajiriwa, iliwachukua miezi mitatu kumaliza kazi katika mashamba ya hekta 20 ya pamba. Siku hizi, baada ya utumiaji wa mashine kwenye shughuli za kulima na kuvuna pamba, ufanisi na mapato yameboreshwa kwa kiasi kikubwa. Mwaka 2020, Amar Aziz alinunua mashine ya kuchuma pamba kwa mkopo, na akanunua mashine nyingine kwa kushirikiana na marafiki yake. "Sasa watu wengi watachagua kuchuma pamba kwa mashine" Amar Aziz amesema. Ratiba ya huduma yake ya uchumaji pamba imepangwa kwa wiki mbili. Ili kuboresha ufanisi wa uvunaji, aliajiri madereva wanne kwa kila mashine. Ukiondoa gharama za mafuta, matengenezo na mishahara ya wafanyakazi, Amar Aziz anakadiria kuwa mashine mbili zake zinaweza kuvuna takriban hekta 533 za pamba na kupata yuan 800,000 (Dola za kimarekani 125,040) mwaka huu. (Xinhua/Ma Kai)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha