Kituo cha ukarimu: kuwawezesha wapeleka vifurushi wapumzike kidogo na kula chakula cha moto

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 08, 2021
Kituo cha ukarimu: kuwawezesha wapeleka vifurushi wapumzike kidogo na kula chakula cha moto

Siku ya Juzi, kwa kuathiriwa na wimbi la baridi, theluji kubwa ilianguka Beijing, na hali ya hewa imekuwa baridi sana. Hata hivyo, wapeleka vifurushi wanaofanya kazi katika nje ya nyumba pia wana kituo cha kupumzika cha kupata ukarimu. Katika eneo la Mashariki la Beijing kuna mgahawa mmoja ambao unawatoa bufee ya mchana ya yuani 12 kwa wapeleka vifurushi. Chakula cha mchana kinaundwa na chakula kikuu na vitoweo vyenye nyama na mboga na kila siku ya wiki kuna orodha ya chakula tofauti. Bufee ya mchana inapewa ruzuka pamoja na Mtaa wa Donghuashi, Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi wa Mitaani, Shirikisho la Biashara na Kampuni ya kupeleka vifurushi. Mkurugenzi wa mgahawa huo alisema, kuanzishwa kwa jiko hilo mwezi Septemba kwa ajili ya wapeleka vifurushi, mgahawa huo unawapokea wapeleka vifurushi zaidi ya 60 kila siku kwa wastani.

Habari zinasema kuwa, katika eneo la Mashariki la mjini Beijing, kama mgahawa huo ulivyofanya, vilivyoanzishwa kwenye migahawa inayokaribu na mitaa na kutoa huduma za ukarimu kwa watu wanaofanya kazi katika nje vimekuwa zaidi ya 360. Vituo hivi vya kutoa huduma za ukalimu vinasaidia watu wanaofanya kazi nje ya nyumba, kama vile wapeleka vifurushi kutatua matatizo ya kutokuwa na mahali panapofaa kula chakula, kunywa maji, kupumzika na kwenda choo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha