Ufaransa yarudisha mabaki 26 ya kale ya utamaduni kwa Benin

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 12, 2021
Ufaransa yarudisha mabaki 26 ya kale ya utamaduni kwa Benin

Saa tisa mchana, Jumatano ya wiki hii, ndege iliyobeba mabaki 26 ya kale ya utamaduni yenye thamani kubwa ilishuka kwenye Uwanja wa Ndege wa Cotonou, Benin. Mamia ya wakazi walikusanyika huko wakicheza ngoma na kuimba nyimbo ili kusherehekea kurejeshwa kwa hazina hizo za kitaifa baada ya miaka 130 iliyopita .

“Tunashuhudia wakati muhimu wa kihistoria. Leo ni siku ya kusisimuka kwa Wabenin wote” alisema Waziri wa Utalii, Utamaduni na Sanaa wa Benin.

Mabaki hayo 26 ya kale ya Utamaduni yalinyang’anywa na jeshi la Ufaransa mwaka 1892 kutoka Dola ya kifalme ya Dahomey, ambayo ni awali ya Jamhuri ya Benin ya hivi leo. Katika mabaki hayo kuna kiti cha kifalme, vinyago na mlango wa kasri ya ufalme ya Dola ya Dahomey.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha