Makala: Maonesho ya utamaduni wa China yafanyika Chuo Kikuu cha Rwanda

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 15, 2021
Makala: Maonesho ya utamaduni wa China yafanyika Chuo Kikuu cha Rwanda
Mmoja wa wanafunzi (Kushoto) akijaribu vazi la asili la China wakati wa Maonesho ya Utamaduni wa China katika Chuo Kikuu cha Rwanda, Chuo Kishiriki cha Elimu cha Kampasi ya Rukara, Mashariki mwa Rwanda, Novemba 10, 2021. Vivutio vinavyoonesha utamaduni wa China vilijaza ukumbi wa wanafunzi katika chuo hicho. Kwa mara ya kwanza yakiandaliwa nje ya Mji Mkuu Kigali, tangu kuzuka kwa virusi vya korona, maonesho hayo kwa mwaka huu yalihusu kujionea utamaduni wa China kama sehemu ya sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Rwanda. (Xinhua/Ji Li)

KIGALI, Rwanda - Vivutio vinavyoonesha utamaduni wa China vilijaza ukumbi wa wanafunzi katika Maonesho ya hivi karibuni ya Utamaduni wa China katika Chuo kishiriki cha Elimu cha Chuo Kikuu cha Rwanda Kampasi ya Rukara, Mashariki mwa Rwanda.

Kwa mara ya kwanza kuandaliwa nje ya Mji Mkuu wa Kigali, tangu kuzuka kwa janga la virusi vya korona, maudhui ya maonesho ya mwaka huu yalihusu kujionea utamaduni wa China kama sehemu ya sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Rwanda.

Maonesho hayo yaliyoandaliwa na Taasisi ya Confucius katika Chuo Kikuu cha Rwanda yalishirikisha vipengele kadhaa, ambapo washindi waliondoka na zawadi. Baadhi ya vipengele muhimu vilivyokuwa sehemu ya maonesho hayo ni: Kuimba mashairi kwa lugha ya Kichina, kuzungumza lugha ya Kichina, kuandika herufi za Kichina, kuonja chai ya Kichina, kuvaa nguo za Kichina, kuimba nyimbo za Kichina, kucheza dansi ya Kichina na kuchora sanaa za Kichina.

Tukio hili liliwavutia wanafunzi wa viwango vyote vya kitaaluma wanaofanya mazoezi ya kuzungumza lugha Kichina au kuandika herufi za Kichina, au ambao walitaka kujifunza zaidi kuhusu utamaduni wa China.

Wanafunzi walivutiwa kwa mara ya kwanza na maonesho ya Kungu-fu yaliyofanywa na vijana kutoka Klabu ya Chow Mantis kutoka Nyamirambo mjini Kigali, na kuhimizwa kushiriki katika michezo mbalimbali ya kiutamaduni wakiongozwa na wanafunzi wengine wa lugha ya Kichina.

Katika ukumbi wa maonesho ya utamaduni, mavazi ya asili ya China yalikuwa moja ya mavazi yaliyovutia zaidi, ambapo wanafunzi walibadilishana kujaribu na kupiga picha.

"Ndiyo, ninafuraha kuvaa vazi hili la Kichina" Concessa Mushimiyimana, mwanafunzi wa hahada ya kwanza wa Hisabati, Biolojia na Elimu aliliambia Shirika la Habari la China, Xinhua, akionesha vazi hilo kwa fahari.

Akizungumza katika hafla hiyo, Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Rwanda, Chuo Kishiriki cha Elimu, Florien Nsanganwimana, aliishukuru Serikali ya China kwa ushirikiano mzuri na serikali ya Rwanda, ambapo alisema bila ya ushirikiano huo uanzishwaji wa Taasisi ya Confucius haungewezekana. 

"Utamaduni ni jambo pana, linalojumuisha maisha yote ya watu. Kila utamaduni una kitu cha pekee cha kujifunza kutoka kwake. Kwa hivyo, tukio hili la maonesho ni fursa ya kufungua mawazo yetu, kutupa yatokanayo na utamaduni wa China. Unaweza kujifunza kutokana na utamaduni wao" alisema.

Zhang Xiaohong, pamoja na Ubalozi wa China nchini Rwanda, aliona kwamba tukio hilo la maonesho ni fursa ya kuwa na mtazamo wa lugha na utamaduni wa China.

"Urafiki kati ya nchi upo katika mshikamano kati ya watu. Mabadilishano ya watu wetu yameongezeka sana, na kujifunza kwa tamaduni hizi mbili kumekuzwa sana" alisema.

Katika kipindi cha nusu karne iliyopita, Rwanda na China zimekuza uhusiano wa pande nyingi na kamili.

“Pia tumeona mifano mingi ya vijana wa Rwanda, waliojifunza lugha ya Kichina na kusoma China, na kutoa mchango mkubwa kwa jamii ya Rwanda,” alisema.

Kwa mujibu wa afisa huyo, uhusiano katika maeneo kuanzia siasa, biashara, uwekezaji, miundombinu, elimu, umekuwa na matokeo ya ajabu, na kwmaba nchi hizo mbili zinajenga uhusiano wa kindugu.

Kwa miaka mingi, mawasiliano kati ya watu na watu yameongezeka sana, ambapo zaidi ya wanafunzi 5,000 wamejiandikisha katika Taasisi ya Confucius katika Chuo Kikuu cha Rwanda, na zaidi ya 2,000 wamesajiliwa na Shirikisho la Kung-Fu Wushu la Rwanda.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha