Wanyamapori adimu walio hatarini kutoweka warejea kuongezeka Chongqing (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 18, 2021
Wanyamapori adimu walio hatarini kutoweka warejea kuongezeka Chongqing

Idara ya Misitu ya Chongqing imeeleza Jumanne ya wiki hii Tarehe 16, kuwa inaharakisha kujenga mfumo wa kusimamia hifadhi ya uoto wa asili na inaendelea kutekeleza mradi wa ulinzi na urejeshaji wa mfumo wa ikolojia .

Kutokana na hatua hizo, makazi ya wanyamapori wa mji mzima yamehifadhiwa vizuri, kundi la wanyamapori adimu walio hatarini kutoweka limeanza tena kuongezeka na matokeo ya kuwahifadhi viumbe anuai yamekuwa dhahiri.

Ikiwa kwenye eneo la mtiririko wa juu wa Mto Changjiang na eneo la Hifadhi ya Mabonde Matatu (Three Gorges Reservoir), Chongqing ni eneo lenye viumbe anuai, pia ni moja ya maeneo muhimu 34 ya hifadhi ya viumbe anuai duniani.

Kwa upande wa hifadhi ya asili, Chongqing imekuwa ikiimarisha hifadhi ya mifumo ya asili ya ikolojia, kama vile misitu, mbuga, mito, maziwa na ardhi oevu, na kuanzisha mfumo wa kisayansi wa kuhifadhi ardhi asili. Katika mji mzima kuna hifadhi za asili 218 za hadhi na aina mbalimbali, zenye jumla ya eneo la mraba karibu hekta milioni 1,269 ambalo linachukua asilimia 15.4 ya eneo lote la mji.

Kwa upande wa urejeshaji wa mfumo wa ikolojia, Chongqing imekuwa ikiimarisha kazi ya kurejesha mfumo wa ikolojia wa misitu na ardhi oevu. Ukubwa wa eneo la misitu unafikia asilimia 52.5 ya jumla ya eneo zima la mji, na mfumo wa ikolojia wa ardhi oevu umeendelea kuimarika zaidi. Katika Bustani ya Ardhi oevu ya Kitaifa ya Hanfeng idadi ya bata bukini wanaoishi katika majira ya baridi ni kati ya 8,000 hadi 20,000.

Kwa upande wa uokoaji na uhifadhi wa wanyamapori adimu walio hatarini kutoweka, Chongqing imekuwa ikiimarisha kikamilifu ulinzi na usimamizi wa wanyamapori muhimu wanaolindwa. Idadi ya tumbili weusi katika Hifadhi ya Kitaifa ya Mlima Jinfo imeongezeka kwa sasa kufikia 150 kutoka idadi ya chini ya 80. Bata jamii ya Mergus squamatus katika majira ya baridi wamekuwa wakiishi katika eneo la Mto Qihe kwa miaka tisa mfululizo na idadi yao imeongezeka kufikia 61 kutoka 35 ya Mwaka 2013.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha