Kongamano la Nne la Urafiki na Ushirikiano kati ya Serikali za Mitaa za China na Afrika lafunguliwa Beijing, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 19, 2021
Kongamano la Nne la Urafiki na Ushirikiano kati ya Serikali za Mitaa za China na Afrika lafunguliwa Beijing, China

Jumanne ya wiki hii, Kongamano la Nne la Urafiki na Ushirikiano kati ya Serikali za Mitaa za China na Afrika lilifanyika hapa Beijing kupitia njia ya mtandao na nje ya mtandaoni. Jukwaa hilo linaandaliwa na Shirika la Urafiki wa Watu wa China kwa nchi za nje (CPAFFC) pamoja na Shirika la Urafiki wa Watu wa China na Afrika.

  Akitoa hotuba ya ufunguzi wa kongamano hilo kwa njia ya video, Waziri Mkuu wa China Li Keqiang alisema, Afrika ni bara lenye matumaini na nguvu. Kwa muda mrefu, China na Afrika zimekuwa zikiungana mkono na kusaidiana, zimeunda urafiki wa kudumu.

Alibainisha kuwa, China iko tayari kuzingatia mahitaji ya Afrika na kuongeza msaada kwa iwezekanavyo wa kutoa chanjo na vifaa vya tiba vya kujikinga dhidi ya virusi vya korona, ili kujenga uimara wa kulinda afya za watu wa Afrika.

Ameongeza kuwa, China ingependa kuoanisha kwa kina mikakati ya maendeleo na Afrika, kutumia nguvu bora za kiuchumi za pande hizo mbili zinazoweza kusaidiana, ili kuhimiza ushirikiano katika sekta halisi uwe wa sifa bora na ufanisi.

Katika kongamano hilo, pande mbalimbali zilisani makubaliano kuhusu kuanzisha uhusiano wa marafiki wa ushirikiano baina ya Mkoa wa Hunan na eneo kubwa la Alaotra-Mangoro la Madagascar, Mji wa Zhengzhou wa Mkoa wa Hunan na Mji wa Ouagadougou wa Burkina Faso na Bandari ya Guangzhou ya Mkoa wa Guangdong na Bandari ya Alexandria ya Misri. Aidha, yalisainiwa makubaliano kuhusu Mkoa wa Liaoning na Wilaya kubwa ya Busoga ya Uganda viwe marafiki wa ushirikaino. Washiriki wa kongamano hilo pia walijadili kuhusu mada tano zinazofuatiliwa pamoja na China na Afrika kuhusuujenzi wa uhusiano wa wa miji marafiki wa ushirikiano, kujiendeleza na kupunguza umaskini, huduma za afya, uvumbuzi na maendeleo, na utawala wa miji.

Kwenye kongamano hilo, washiriki walijadilia zaidi mada kuu, wakishauriana kwa kina na kupanga kufanya kazi pamoja kwa mustakabali wa baadaye. 

Waziri wa Muungano na Mambo ya Jadi wa Afrika Kusini, Nkosazana Dlamini-Zuma wakati akizungumzia ujenzi wa miji marafiki wa ushirikiano kati ya China na Afrika alisema, ushirikiano kati ya serikali za mitaa ni nguvu kubwa inayohimiza kazi ya kutimiza Ajenda ya Mwaka 2063 ya Umoja wa Afrika.

Kwa upande wake, Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Watoto wa Zanzibar, Tanzania Nassor Ahmed Mazrui akizungumzia ushirikiano katika sekta ya afya alisema, Tanzania inashughulikia mradi wa kukinga na kudhibiti ugonjwa wa kichocho chini ya msaada wa upande wa China. Aliongeza kuwa, Tanzania inaishukuru China kwa msaada wa kiufundi na kiujuzi, pamoja na msaada wa chanjo dhidi ya virusi vya korona. 

Kongamano la Ushirikiano kati ya Serikali za Mitaa za China na Afrika lilianzishwa na Shirika la Urafiki wa Watu wa China kwa nchi za nje mnamo Mwaka 2012. Ni kongamano muhimu chini ya utekelezaji wa malengo ya Baraza la Ushirkiano la China na Afrika (FOCAC). Kongamano la mwaka huu limefanyika kwa wakati uliopangwa likishinda athari ya janga la korona, na limechangia Mkutano wa Nane wa Mawaziri wa Baraza la Ushirikiano la China na Afrika utakaofanyika huko Senegal. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha