Zhaosu Xinjiang: Mifugo mingi yahamia kwenye malisho mapya (5)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 19, 2021
Zhaosu Xinjiang: Mifugo mingi yahamia kwenye malisho mapya

Ifikapo Novemba ya kila mwaka, hali ya hewa huanza kuwa ya baridi. Uhamaji wa majira ya baridi wa mifugo 180,000 katika Wilaya ya Zhaosu mkoani Xinjiang umeanza. Wafugaji wanatumia magari kuongoza mifugo yao kuhama kutoka malisho ya majira ya mchipuko na mpukutiko yaliyoko Mlima Wusun kwenda kwenye malisho ya majira ya baridi yaliyoko kwenye mabonde makubwa ya Ahe Yazi, ambayo hayafunikwi na theluji, na mifugo inaweza kutafuta malisho na kuishi huko katika majira ya baridi kwa usalama.

Hapo kabla, wafugaji walikuwa wanatumia farasi kubeba mizigo yao yote. Siku hizi, kutokana na kuboreshwa kwa hali ya maisha, wakati wa kuhama wafugaji wengi wanakodi magari kusafirisha kwanza mizigo mikubwa ya nyumbani kwenye malisho ya sehemu nyingine. Kwa hiyo wakati wa kuhama, wanaandaa chakula na nyumba ya muda tu na kuweza kusafiri kirahisi.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha