Shukrani kwa kisimbuzi cha kidijitali , tumeunganishwa na Dunia (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 22, 2021
Shukrani kwa kisimbuzi cha kidijitali , tumeunganishwa na Dunia
Kampuni ya StarTimes ilifanya semina ya mafunzo nchini Kenya Mwaka 2018. (China Daily)

Televisheni ya satelaiti ikiwa moja ya miradi ya “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, imebadilisha maisha ya Waafrika wengi.

Katika miaka mitatu iliyopita, ingawa amemiliki televisheni, George Waweru alikuwa bado hajaweza kutazama televisheni kwa kuwa hakuwa na uwezo wa kununua kisimbuzi, Kwa hiyo, alipopewa bure kisimbuzi cha kidijitali cha juu ya televisheni na kampuni moja ya China Mwaka 2018, maisha yake yamebadilika.

Waweru mwenye umri wa miaka 48 ni baba wa watoto watatu amesema: “sasa ninaweza kutazama vipindi vingi mbalimbali vya nchini na vya nje hivyo inaniwezesha mimi kupata habari na burudani kama wakazi wa mjini.” Waweru analipa pesa sawa na dola za Marekani 4.5 kila mwezi na anaweza kutazama makumi ya vipindi vikiwemo habari za kimataifa na filamu za karate za China, pia watoto wake wanaweza kutazama vipindi vya katuni kupitia masafa mbalimbali.

Kama ilivyo kwa Waweru, watu wengi wanaoishi katika maeneo ya pembezoni nchini Kenya na nchi nyingine za Afrika, maisha yao yamebadilika baada ya kuunganishwa na Dunia kupitia televisheni ya satelaiti. Mabadiliko hayo yote ni kutokana na utekelezaji wa mradi mmoja, ambao umekuwa ukiunganisha vijiji 10,000 vya nchi 25 za Kusini mwa Jangwa la Sahara na televisheni ya satelaiti.

William Masy, Mkurugenzi wa Uhusiano wa Kampuni ya StarTimes Group, inayotekeleza mradi huo amesema, mradi huo ni moja ya mpango wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, unawawezesha wakazi wa sehemu za pembezoni hususan maeneo ya vijijini barani Afrika kupata uhakika wa kudumu wa kupata habari kutoka sehemu mbalimbali za Dunia. Umepunguza pengo la kupata habati za kidijitali kati ya miji na vijiji vya Afrika.

Amesema, hadi kufikia mwishoni mwa Mwezi Agosti, mradi huo ambao China iliahidi katika Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika lililofanyika Johannesburg, Afrika Kusini umekamilika katika vijiji 8612 vya nchi 20, zikiwemo Burundi, Ghana, Guinea, Kenya, Madagascar, Malawi, Msumbiji, Rwanda, Senegal, Uganda na Zambia. Watu zaidi ya milioni 6.5 wanaweza kutumia televisheni ya satelaiti.

Kwa upande wake Guo Ziqi, Naibu Meneja Mkuu wa StarTimes Group, anasema mradi wa televisheni ya satelaiti kwa vijiji 10,000 vya Afrika umewanufaisha sana wakaazi katika maeneo mengi ya pembezoni ya Afrika.

"Mradi huu umepata kutambuliwa na kuthaminiwa sana katika nchi unakotekelezwa, na katika nchi nyingi marais au maafisa wengine wakuu kama mawaziri wameshiriki kwenye sherehe za uzinduzi ili kuonesha uungaji mkono wao. Katika baadhi ya nchi, TV za satelaiti zilitumika kwa kiasi kikubwa katika miji mikuu, lakini sasa inapatikana katika maeneo mengi ya vijijini.

"StarTimes inatarajia kufanya kazi na wadau mbalimbali ndani na nje ya nchi ili kuzalisha vipidi vingi vya TV vinavyokidhi mahitaji ya Waafrika, kama vile vipindi vya mafunzo ya kilimo na elimu ya afya." 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha