Lugha Nyingine
Rais wa China aendesha mkutano wa kuadhimisha miaka 30 tangu China na ASEAN zianzishe utaratibu wa mazungumzo
(CRI Online) Novemba 23, 2021
Rais Xi Jinping wa China jana asubuhi kwa njia ya video alihudhuria na kuendesha mkutano wa kilele wa kuadhimisha miaka 30 tangu China na Umoja wa Nchi za Kusini Mashariki mwa Asia (ASEAN) zianzishe utaratibu wa mazungumzo.
Kwenye mkutano huo rais Xi alisisitiza kuwa China daima itaendelea kuwa jirani mwema, rafiki mkubwa na mwenzi mzuri wa ASEAN, na itashikilia kutoa kipaumbele kwa Umoja huo katika mambo yake ya kidiplomasia. Alisema China pia inaunga mkono kithabiti mshikamano na ujenzi wa Umoja huo, kuunga mkono hadhi kuu ya kikanda ya Umoja huo, na kuunga mkono Umoja huo kuonesha umuhimu wake mkubwa zaidi katika mambo ya kikanda na kimataifa.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma