“Baba wa Juncao” Lin Zhanxi: Kunufaisha maisha ya watu kwa kupitia “Ukanda Mmoja, Njia Moja” (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 24, 2021
“Baba wa Juncao” Lin Zhanxi: Kunufaisha maisha ya watu kwa kupitia “Ukanda Mmoja, Njia Moja”
Lin Zhanxi (wa kwanza kutoka kulia) alipotoa mafunzo ya teknolojia ya Juncao alipigwa picha pamoja na wakazi huko Afrika Kusini. (Picha ilipigwa Machi, 2005)

Lin Zhanxi, mwanasayansi mkuu wa Taasisi ya kitaifa ya teknolojia ya Mradi wa Juncao katika Chuo Kikuu cha Kilimo na Misitu cha Fujian, alivumbua teknolojia ya Juncao katika miaka ya 1980, ambayo inatumia nyasi badala ya ubao kwa kuzalisha uyoga, na kutatua tatizo la kutumia miti mingi kwenye mchakato wa kuzalisha uyoga. Teknolojia hiyo inatumika sana nchini na nje, kwa hivyo Profesa Lin anasifiwa kuwa “Baba wa Juncao”.

Teknolojia hiyo inawezesha nyasi kuzalisha uyoga na kuongeza kipato, kupunguza athari ya upepo mkali na mchanga mwingi, kulisha mifugo, na pia kutumika katika kuzalisha umeme na kutengeneza karatasi. Hivi sasa teknolojia hiyo imeenezwa kwa nchi zaidi ya 100, ikijulikana kuwa“nyasi za furaha” na “nyasi za China”.

Profesa Lin alisema, “Hivi sasa Juncao inapendwa sana na watu wa nchi na maeneo ya ‘Ukanda Mmoja, Njia Moja’. Teknolojia ya Juncao inapendeza na kuhitaji nafasi ndogo tu, ikiweza kupata ufanisi kwa haraka, hivyo gharama ya kutembeza teknoljia hiyo ni ndogo. Tekonojia hiyo imetoa njia mpya kwa ajili ya nchi zinazoendelea kuondokana na umaskini na kupata maendeleo endelevu.”

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha