Chuo Kikuu cha Dakar chaweka kozi ya kwanza ya Lugha ya Kichina nchini Senegal (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 25, 2021
Chuo Kikuu cha Dakar chaweka  kozi ya kwanza ya Lugha ya Kichina nchini Senegal
Hapa ni nje ya Chuo cha Confucius katika Chuo Kikuu cha Dakar. Picha ilipigwa Jumanne ya wiki hii.

Chuo Kikuu cha Dakar cha Senegal kilifanya mkutano wa kutangaza kozi yake ya Lugha ya Kichina Jumanne ya wiki hii kwenye Chuo chake cha Confucius. Hali hiyo inamaanisha somo la lugha ya Kichina limeingia rasmi kwenye mfumo wa elimu ya juu ya Senegal.

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dakar alisema kwenye mkutano huo kuwa, kuwekwa kwa kozi ya Lugha ya Kichina katika Chuo cha Lugha ya matumizi katika Chuo kikuu hicho kuna umuhimu mkubwa kwa kueneza elimu ya Lugha ya Kichina nchini Senegal, na kutaongeza sana mvuto wa somo la Lugha ya Kichina kwa wanafunzi.

Mkuu wa Chuo cha Confucius wa upande wa China Cui Jie alisema, kwa kufuata utekelezaji wa pendekeo la “Ukanda Mmoja, Njia moja” katika Senegal na Afrika ya Magharibi, mahitaji ya nchi hiyo kuhusu watu wenye ujuzi wa lugha ya Kichina yamekuwa makubwa sana, kuwekwa kwa kozi hiyo kutasaidia kuwaandaa watu wengi zaidi wenye ujuzi kwa ajili ya ushirikiano na mawasiliano kati ya China na Senegal.

Chuo cha Confucius katika Chuo Kikuu cha Dakar kilianzishwa mwishoni mwa mwaka 2012, kinaendeshwa na Chuo kikuu cha Dakar pamoja na Chuo Kikuu cha Liaoning cha China, kikiwa ni Chuo cha Confucius cha kwanza kilichoko katika Afrika ya Magharibi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha