Mtaalam wa Uchumi asema Uchumi imara wa China kuvutia uwekezaji na watu wenye vipaji kutoka nchi za nje

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 26, 2021
Mtaalam wa Uchumi asema Uchumi imara wa China kuvutia uwekezaji na watu wenye vipaji kutoka nchi za nje
Picha iliyopigwa Novemba 3, 2020 ikionesha gati ya kontena ya Bandari ya Yangshan iliyoko Shanghai, Mashariki mwa China (Xinhua/Wang Xiang)

LONDON - Dan Wang, Mtaalam Mkuu wa Uchumi katika Benki ya Heng Seng (China) amesema, uchumi wa China ulioimarika utavutia uwekezaji mkubwa na watu wenye vipaji kutoka nje ya China.

"Kivutio kikuu cha China kwa uwekezaji wa kigeni ni ukuaji imara wa uchumi," Wang ameandika katika maoni yaliyochapishwa hivi karibuni kwenye Gazeti la Financial Times, huku akibainisha kuwa ukuaji wa uchumi wa China ni tofauti kabisa na uchumi wa maeneo mengine ya Dunia.

"Hakuna shaka kwamba ongezeko la Pato la Taifa la mwaka huu litazidi lengo lililowekwa na Serikali la zaidi ya asilimia 6. Tunakadiria kuwa ongezeko la mwaka mzima linatarajiwa kuzidi asilimia 8," ameandika.

Kwa mujibu wa Wang, takwimu zinaonesha kuwa uwekezaji wa kigeni haujapungua nchini China na sera ya kufungua soko la ndani haijabadilika pia.

Amesema kuwa, uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje (FDIs) kwa ujumla duniani ulipungua Mwaka 2020, lakini uwekezaji huo nchini China uliendelea kukua. Kwa mujibu wa Wang, Mwaka 2020, FDI ya China ilichangia zaidi ya moja ya tano ya jumla ya uwekezaji wa Dunia, ikiwa ni mara mbili ya uwekezaji wake wa kabla ya janga la UVIKO-19, na hali hii itaendelea mwaka huu.

Wang amebainisha kuwa, wasiwasi kuhusu ongezeko la uchumi wa China katika siku za usoni unatokana hasa na kushuka kwa sekta ya nyumba. Hata hivyo, uwekezaji katika sekta ya viwanda utapunguza athari.

Kwa mujibu wa takwimu rasmi za Serikali, Pato la Taifa la China (GDP) lilikua kwa asilimia 4.9 katika robo ya tatu ya mwaka huu, ikiwa ni ongezeko dogo kuliko ukuaji wake wa asilimia 18.3 katika robo ya kwanza na asilimia 7.9 katika robo ya pili. Katika robo tatu za kwanza za mwaka huu, pato la nchi lilipanuka kwa asilimia 9.8, ambalo ni juu kuliko lililotarajiwa la asilimia 6. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha