Vituo vya China vya uchunguzi wa hali ya hewa kwenye Ncha ya Kusini ya Dunia vyaanza kuendesha kazi rasmi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 02, 2021
Vituo vya China vya uchunguzi wa hali ya hewa kwenye Ncha ya Kusini ya Dunia  vyaanza kuendesha kazi rasmi

Habari kutoka Idara ya Hali ya Hewa ya China zilisema, Kituo cha habari za hali ya hewa cha China kimepokea tarakimu kuhusu hali ya hewa zilizotolewa na vituo vya Kunlun na Mlima Tai katika Kituo cha Uchunguzi cha China kwenye Ncha ya Kusini ya Dunia Novemba 30 saa mbili jioni. Hali hiyo inamaanisha baada ya uendeshaji tulivu wa miaka 5 na miaka 9, vituo hivyo viwili vimekuwa na uwezo wa kuendesha kazi, na kuanzia Jumatano ya wiki hii, vituo hivyo viwili vimeendesha kazi rasmi, ambapo vitatoa tarakimu mfululizo kuhusu uchunguzi wa hali ya hewa kwa muda mrefu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha